Sio kila mtu atakuelewa kwa mara ya kwanza utakapomuambia au atakapokusikia.
Kuna watu wengi sana wanakata tamaa kwa sababu kuna mtu walitarajia awaelewe na awasapoti ila walipokutana naye hawakufanya hivyo.
Hii ni kawaida, wala isikukatishe tamaa kabisa.
Kuna watu itachukua muda sana kukuelewa.
Usiwachukie wala usiwalalamikie, inawezekana hata ingekuwa wewe ungechelewa pia.
Kama una wazo, kipaji au biashara.
Ni lazima uwe na uwezo wa kukabiliana na HAPANA nyingi iwezekenavyo bila kukata tamaa kabisa.
Usiogope kukataliwa, ni sehemu ya kuelekea kukubaliwa.
Unaikumbuka ile kanuni niliwahi kukufundisha ya SWSWSWSW (Someone Won’t, Someone Will, So What Someone is waiting).
Mwingine atakataa, mwingine atakubali, wewe usijali, kuna mtu ANAKUSUBIRI huko mbele).
USIKUBALI HAPANA MOJA IKATISHE NDOTO YAKO!