Ndonya kwa wamakonde ilikuwa silaha ya kujilinda

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
makonde_tanzania_kaobanga.jpg
WAMAKONDE na Wameto wa Msumbiji wanaishi katika Mkoa wa Cabo Delgado Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo na Wamakonde wa Tanzania wanaishi zaidi katika wilaya zote za Mkoa wa Mtwara ila Masasi na Nanyumbu wapo kwa asilimia ndogo na huishi na wenyeji wao Wamakua na Wayao.

Wamakonde wamejipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na kuwa na ukakamavu na shughuli za uchongaji wa vinyago. Tofauti kubwa kati ya Wamakonde wanaoishi Kusini mwa Mto Ruvuma (Msumbiji) na Kaskazini mwa Ruvuma (Tanzania) ni aina ya urembo wa ndonya. Wale wa Msumbiji wana ndonya ndogo juu ya midomo yao wakati wa Tanzania wana ndonya kubwa zaidi midomoni mwao.

Wamakonde huonekana kwa uzuri wao, wapo waliochanja sehemu za juu ya mdomo, masikio na uso. Inaaminika kuwa chanzo cha kuchanja, kutoboa midomo na kuweka ndonya ilikuwa kujilinda dhidi ya wafanyabiashara wa watumwa ambao walibeba watumwa kwenda kwenye mashamba huko Ulaya.

Ndonya na chanjo ziliwakasirisha sana wafanyabiashara wa Kiarabu kwa kuona kuwa watu hao hawapendezi. Wamakonde wengine wa Msumbiji waliamua kuchonga meno yao, ili kujilinda, kwamba mtu ambaye angeingia katika himaya yao akiwa hajachanja, hana ndonya na hajachonga meno, walimuona ni adui yao na kama ni mweusi, ni mpelelezi wa Waarabu ili wavamie kuwachukua kwenda utumwani.

Tabia hizi zikawa ni desturi na mila zao na zikawa kama urembo ndani ya kabila la Wamakonde. Baada ya kukomeshwa kwa biashara ya watumwa, mila hizi zilianza kutoweka na wengi wameachana nazo.
 
Huu uzi ndo umeishia hapa?
 
Ungetuwekea na picha kati ya hao wamakonde Wa Nchumbiji na Wa hapa Tz ili tujionee! Vipi kuhusu zile chale zao za usoni?
Nalog off
 
Jino lililochongwa ilikua ni njia ya kumpatia dawa na chakula(uji mwepesi) mgonjwa wa tetenus enzi hizo baada ya kukaamaa na kushindwa kufungua kinywa
 
makonde_tanzania_kaobanga.jpg
WAMAKONDE na Wameto wa Msumbiji wanaishi katika Mkoa wa Cabo Delgado Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo na Wamakonde wa Tanzania wanaishi zaidi katika wilaya zote za Mkoa wa Mtwara ila Masasi na Nanyumbu wapo kwa asilimia ndogo na huishi na wenyeji wao Wamakua na Wayao.

Wamakonde wamejipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na kuwa na ukakamavu na shughuli za uchongaji wa vinyago. Tofauti kubwa kati ya Wamakonde wanaoishi Kusini mwa Mto Ruvuma (Msumbiji) na Kaskazini mwa Ruvuma (Tanzania) ni aina ya urembo wa ndonya. Wale wa Msumbiji wana ndonya ndogo juu ya midomo yao wakati wa Tanzania wana ndonya kubwa zaidi midomoni mwao.

Wamakonde huonekana kwa uzuri wao, wapo waliochanja sehemu za juu ya mdomo, masikio na uso. Inaaminika kuwa chanzo cha kuchanja, kutoboa midomo na kuweka ndonya ilikuwa kujilinda dhidi ya wafanyabiashara wa watumwa ambao walibeba watumwa kwenda kwenye mashamba huko Ulaya.

Ndonya na chanjo ziliwakasirisha sana wafanyabiashara wa Kiarabu kwa kuona kuwa watu hao hawapendezi. Wamakonde wengine wa Msumbiji waliamua kuchonga meno yao, ili kujilinda, kwamba mtu ambaye angeingia katika himaya yao akiwa hajachanja, hana ndonya na hajachonga meno, walimuona ni adui yao na kama ni mweusi, ni mpelelezi wa Waarabu ili wavamie kuwachukua kwenda utumwani.

Tabia hizi zikawa ni desturi na mila zao na zikawa kama urembo ndani ya kabila la Wamakonde. Baada ya kukomeshwa kwa biashara ya watumwa, mila hizi zilianza kutoweka na wengi wameachana nazo.
Sisi tuna mawazo ya corona wewe unalete story ambazo hazitusaidii na hili janga!!
 
Haya wadau leteni basi sifa kuu za watoto wa kimakonde,kimakua na wayao
 
Wamakonde waliwaogopa wababe zao Wandengereko waliokuwa wakiwamata na kuwauza utumwa kwa waarabu
 
Mkuu
makonde_tanzania_kaobanga.jpg
WAMAKONDE na Wameto wa Msumbiji wanaishi katika Mkoa wa Cabo Delgado Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo na Wamakonde wa Tanzania wanaishi zaidi katika wilaya zote za Mkoa wa Mtwara ila Masasi na Nanyumbu wapo kwa asilimia ndogo na huishi na wenyeji wao Wamakua na Wayao.

Wamakonde wamejipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na kuwa na ukakamavu na shughuli za uchongaji wa vinyago. Tofauti kubwa kati ya Wamakonde wanaoishi Kusini mwa Mto Ruvuma (Msumbiji) na Kaskazini mwa Ruvuma (Tanzania) ni aina ya urembo wa ndonya. Wale wa Msumbiji wana ndonya ndogo juu ya midomo yao wakati wa Tanzania wana ndonya kubwa zaidi midomoni mwao.

Wamakonde huonekana kwa uzuri wao, wapo waliochanja sehemu za juu ya mdomo, masikio na uso. Inaaminika kuwa chanzo cha kuchanja, kutoboa midomo na kuweka ndonya ilikuwa kujilinda dhidi ya wafanyabiashara wa watumwa ambao walibeba watumwa kwenda kwenye mashamba huko Ulaya.

Ndonya na chanjo ziliwakasirisha sana wafanyabiashara wa Kiarabu kwa kuona kuwa watu hao hawapendezi. Wamakonde wengine wa Msumbiji waliamua kuchonga meno yao, ili kujilinda, kwamba mtu ambaye angeingia katika himaya yao akiwa hajachanja, hana ndonya na hajachonga meno, walimuona ni adui yao na kama ni mweusi, ni mpelelezi wa Waarabu ili wavamie kuwachukua kwenda utumwani.

Tabia hizi zikawa ni desturi na mila zao na zikawa kama urembo ndani ya kabila la Wamakonde. Baada ya kukomeshwa kwa biashara ya watumwa, mila hizi zilianza kutoweka na wengi wameachana nazo.
Mkuu, Sidhani kama ni kweli kwamba ni sababu ya kujilinda. Ninacho fahamu ni kwamba Ndonya na Zile Chale ni sababu ya Urembo tu na kuwavutia wanaume. Ndo maana huwezi kukuta Mwanaume wa Kimakonde kaweka Ndonya, labda chale tena kwa wachache sana. Sababu ya wamakonde wengi kutochukuliwa utumwani ni kutokana na asili yao ya maisha ambapo hawakua na mfumo wa utawala wa kichifu kama ilivyo kwa makabila mengine. Mwanaume akishaanza kujitegemea anahama anaenda kuanzisha makazi na familia yake sehemu porini. Ni kama vile maisha ya Bushmens. So kupata watumwa ilikua ishu sana kuwapata coz wametawanyika. Ndonya ilikua kivutio wakat wa ngoma au sherehe za unyago. Hayo ni machache niyajuayo
 
Back
Top Bottom