Rai Pazzy
JF-Expert Member
- Jul 6, 2015
- 493
- 187
Leo nimeota ndoto ambayo ipo hivi;
Kulikuwa kuna mtu alikuwa anafanya mapenzi na dada mmoja hivi chumba cha pili. Baada ya kumaliza akaingia kaka wa yule dada na kumkuta dada yake kashafanya mapenzi. Ghafla yule aliyefanya nae mapenzi akatokea kwa nyuma na kuanza kumwita yule dada baby, baby!
Cha ajabu yule dada akageuka kwa sura ya kutisha (jini) na kucheka kicheko cha Shumileta, kilichofuata ni kukatwa kichwa kwa yule kaka aliyefanya nae mapenzi halafu akachukua kile kichwa na kukizika, hapo nikashtuka.
Niliposhtuka nikaanza kusoma quran a'udhu zote mbili mara 3/3, na quran huwa 'llahu mara 3, ayat qursi *3, ghafla baada ya kuanza kusoma nikasikia kishindo juu ya paa nikasema qafakka rabbuka kisha nikalala.
Baada ya muda kupita ile ndoto ikaendelea kwa mimi kumwambia mke wangu kuwa ana mke mwengine so hatakiwi kumwogopa ila sikuangalia nyuma. Kumbe yule mwanamke alikuwa kwenye gari langu na mke wangu akawa anamwona ndo akaniambia si yule pale? Ile kugeuka yule mwanamke akapotea na kuja nyuma yangu, hapo nikahisi kama kuna mtu kanisimamia nyuma.
Baada ya kuhisi kama kuna mtu kanisimamia nikajaribu kujiinua (hapo ndoto ishaisha niko kwenye akili za kawaida) lakini nikashindwa huku mwili ukinisisimka vibaya mno. Nikaanza kusoma tena ayat qursii na mdomo nao ukawa haunyanyuki ndipo nikaanza kusoma bila kunyanyua mdomo (kimoyomoyo), zilipofika ayat qursii 3 nikaunganisha na dua moja hii inaitwa qafakka rabbukka, na zilipofika 3 nikahisi kama nimeachiwa hivi.
Baada ya hapo nikajaribu kutikisa kidole nikaona kinacheza, maana mpaka kidole kilikuwa hakichezi, nikakurupuka na kuanza kumtaja Mungu kwa jina la ALLAHU AKBAR wakati namtaja Mungu nikasikia nasisimka mwili na nikasikikia komeo la mlango wa nje linacheza kama kuna mtu anatoka nje.
Tangu hapo sijalala, ilikuwa saa 9:32 mpaka naandika hii thread sijalala kabisa, so kama kuna mtu ana uelewa wa haya mambo naomba anifafanulie maana naogopa vibaya mno.
Nawasilisha wakuu.