Ndoto hizi zimenichosha

Ndoto hizi zimenichosha

Masalia Mpya

Member
Joined
Mar 24, 2023
Posts
53
Reaction score
68
Habari zenu kwa ujumla

Nimekuwa nikiota ndoto zinazofanana fanana.

Iko hivi mimi naishi Dodoma, ila ni mwenyeji wa Lindi. Nimezaliwa huko na kusoma huko mpaka secondary. Chuo nikatoka kwenda mikoa mimgine. Kuanzia hapo nikawa narudi Lindi kama mgeni. Miaka 5 nyuma tulihamisha makazi na kuhamia Mtwara, yaani familia nzima walihama kwa hiyo Lindi tunakwenda kama wageni.

Sasa hivi nina familia yangu huku Dodoma naendelea na maisha yangu, hata nikienda kwetu Mtwara pia naenda kama mgeni siku chache naondoka.

Ndoto zinazonisumbua ni hizi, yaani kwa week mara 2 au 3 naota niko ambako tulishahama, maisha yanaendelea hapo Lindi. Kama ni misiba/ sherehe/ maisha ya familia yetu/ mtaani naota niko Lindi niko na majirani wa Lindi, ndugu walioko Lindi yaani kama vile hatujahama.

Sijawahi kuota niko Mtwara tuliko hamia, hata nikiota wazazi wangu au ndugu zangu naota tuko nyumbani Lindi.

Nashindwa kuelewa, mbona sioti nikiwa Dodoma au Mtwara? Mbona huku nina majirani na hata ndugu wengine Dodoma na Mtwara ila nawaota walioko Lindi? Kwa kweli zimenichosha.

Naombeni ushauri
 
NAFSI Yako imefungwa huko, Kwa ufupi Kwa kuwa umefungiwa huko,

Inahitaji msaada Ili utoke kifungoni ndipo uhame Rasmi.
 
Kuna kitu kilitokea huko kikakuathiri sasa bado huja ki solve ndo maana unaota sana ndoto ukiwa huko
 
Nafsi inakumbuka kwao ilipo zaliwa na kukulia hakuna jipya hapo zaidi, Baada ya muda nafsi itazowea makaazi mepya na kutulia.
 
mi tangu 2014 nimeondoka mkoani na sijawahi kurudi, ila mpaka leo ndoto hizo zinanijia hapo hakuna cha nafsi kuzoea wala kusahau kuna maana yake kiroho
 
Kuna kitu kilikuvutia sna huko lindi, ndio maana akili yako ina kumbukumbu nzuri za lindi.
 
Habari zenu kwa ujumla

Nimekuwa nikiota ndoto zinazofanana fanana.

Iko hivi mimi naishi Dodoma, ila ni mwenyeji wa Lindi. Nimezaliwa huko na kusoma huko mpaka secondary. Chuo nikatoka kwenda mikoa mimgine. Kuanzia hapo nikawa narudi Lindi kama mgeni. Miaka 5 nyuma tulihamisha makazi na kuhamia Mtwara, yaani familia nzima walihama kwa hiyo Lindi tunakwenda kama wageni.

Sasa hivi nina familia yangu huku Dodoma naendelea na maisha yangu, hata nikienda kwetu Mtwara pia naenda kama mgeni siku chache naondoka.

Ndoto zinazonisumbua ni hizi, yaani kwa week mara 2 au 3 naota niko ambako tulishahama, maisha yanaendelea hapo Lindi. Kama ni misiba/ sherehe/ maisha ya familia yetu/ mtaani naota niko Lindi niko na majirani wa Lindi, ndugu walioko Lindi yaani kama vile hatujahama.

Sijawahi kuota niko Mtwara tuliko hamia, hata nikiota wazazi wangu au ndugu zangu naota tuko nyumbani Lindi.

Nashindwa kuelewa, mbona sioti nikiwa Dodoma au Mtwara? Mbona huku nina majirani na hata ndugu wengine Dodoma na Mtwara ila nawaota walioko Lindi? Kwa kweli zimenichosha.

Naombeni ushauri
Ndiyo hiyo inamaanisha watu ulioishi nawo wanakwazika kwa kitendo cha wewe kuishi maisha yako mengine kwani yanayofanyika ndani ya familia ni mambo mengi sana, sali sana MUNGU ALIYE HAI AKITOE MAZINGIRA HAYO NA AKULETE MAZINGIRA YA SASA Keanu ukiota hivyo humaanisha utarudi nyuma kimaisha hautasonga, kama ulikuwa unatumiwa vibaya bado uko kifungoni mwombe MWENYEZI MUNGU ALIYE HAI AFUNGUE VIFUNGO ILI UISHI MAISHA YASASA
 
Your village people in Lindi want you back.
 
Lindi sehemu gani mkuu aisee tumebadilishana me home Dom Dom huko ila now makazi Lindi beach... Iko hivyo kwenye ndoto hata mimi huwa naota mambo ya sekondar ila chuo na primary siotagi
 
Back
Top Bottom