Ndoto na uhalisia katika Mahusiano

Ndoto na uhalisia katika Mahusiano

soam

Member
Joined
Jan 23, 2013
Posts
31
Reaction score
8
Mahusiano ni mazuri pia ni matamu, mke mkarimu na unyenyekevu usioshaka, anayeheshimu na kujali mwenye upendo na huruma, asiye mpinzani wala mshindani anayeridhika na kushukuru, akijishusha na kujidunisha mahusiano kuyaboresha. Mpewa zawadi na kushukuru asiyekosoa kabla ya kushukuru, maana kwake ni bidhaa adimu hata kuonyesha nia, anaunganisha watoto na baba yao huwaambia mazuri yake.

Tingatinga mtengeza njia huondoshwa asiiharibu, majukumu ni wajibu, wajibu huleta wajibu, mtimiziwa lipo jambo lapaswa alitimize, barabara imekamilika tingatinga imeondoshwa.

Maisha ni kuchagua nasi tumechaguana, furaha ngumu kuchagua hukesha tukiitafuta, vipaumbele huchaguliwa vya kwetu ni vipi kwani?

Maisha ni furaha tengeneza mazingira ya furaha, omba furaha yako tafuta furaha yako. Tengeneza kwa familia yako omba kwa familia yako, tafuta kwa ajili yako japo yapo mashaka. Tengeneza asubuhi kisha omba mchana, tafuta jioni sana kwa kuchelewa waweza fika.

Furahisha jamii yako furahisha familia yako, furahisha nafsi yako. Furaha lazima ipatikane, furaha muhimu ipatikane, furaha lazima kuishi.

“Na wewe furaha haipo, bila wewe dunia haipo”

“Maisha Bila Furaha ni Safari Isiyoeleweka”
 
Hii kitu imekaa kama malenga vile. Bado naisoma na kuitafakari ila nahisi natumia nguvu nyingi sana. Mtoa mada uwe unalainisha kidogo.
 
Hii kitu imekaa kama malenga vile. Bado naisoma na kuitafakari ila nahisi natumia nguvu nyingi sana. Mtoa mada uwe unalainisha kidogo.
Inaonekana ni mdau wa malenga wapya..
 
Hakika umenena vyema... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...




Cc: mahondaw
 
Hii kitu imekaa kama malenga vile. Bado naisoma na kuitafakari ila nahisi natumia nguvu nyingi sana. Mtoa mada uwe unalainisha kidogo.
Sawa, ila vipengele vyepesi kuelewa.
 
hivi hawa .com wapo wa hivyo mkuu mpewa na kushukur
 
FB_IMG_1604128189666.jpg
 
Back
Top Bottom