NDOTO: Rais Magufuli kutawala awamu moja tu...

Mkuu achana nao hiyo ndoto ni ya mchana kweupe anaanzaje kuachia uenyekiti mpaka mwingine aje awe mgombea? Upinzani wenyew hauaminiki magufuli ni forever mpaka 2025
 
Mazuri yapi Mzee?
Hajatoa mkopo kwa mwanafunzi ata mmoja aliyewahi kupita private schools.
Amebana pesa na hakuna biashara inayoenda vizuri mtaani.
Tangia mwaka Jana mpaka sasa bei za vitu zimepanda karibia Mara mbili.
Sembe 25kg inauzwa 39000 kutoka 19000 na amenyamaza kama haoni.
Amezima matangazo ya bunge live bila sababu za msingi,
Hajatoa ajira ilihali kuna sekta kibao zinaupungufu.
Unamsifia kwa mazuri gani kaka?
Million 50 kwa kila kijiji au?
Tanzania ya viwanda au?
Kupanda kwa ushuru kila sehemu au?
Acha mahaba ndugu leta facts, wanamsifia kwasababu hawajui tunavyotaabika .
Kesi zenyewe za bandarini na akina masamaki hatujui zimeishia wapi?
Hakuna fisadi ata moja lililokanatwa au kufilisiwa, ww unataka tumusifie kwa lipi?
 

Mazuri km yapi ebu yataje?
 
Lala tena uote, jamaa anapiga kazi tu kutimiza aliyoahidi. Kwa mujibu wa katiba mkataba wake ni awamu moja tu (5 yrs), hiyo awamu nyingine unaiota wewe.
 

Akikujibu uniite watu wengine km wamelewa vile wkt wa kucoment eti amefanya mazuri mazuri atuambie hapa?
 
Na unajiita great thinker toka lini ndoto zikawa kweli basi ota uwe Bakhresa au uwe trump na tuone iwe kweli
 
Binafsi naona kabisa nchi hii imemshinda na akisema anajiuzulu watu wengi watafurahi sana .
Hajatoa ajira mpya na ilihali sekta kibao zinamapungufu.
Amebana sana pesa mtaani kiasi kwamba hakuna biashara inayoenda vizur.
Vitu vimepanda bei karibia Mara mbili mfano sembe 25kg inauzwa 38000 kutoka 19000.
Hajatoa mkopo kwa mwanafunzi ata mmoja aliyewahi kupita private school ata kama alisomeshwa kwa msaada.
Amezima matangazo ya bunge bila sababu yoyote ya mhimu.
Hakuna fisadi lolote alilokamata wala kulitaifisha Mali.
Zile million 50 zilikuwa porojo tu, maana yake tulidanganywa.
Me naona anasitahili kukaa chini ya mtu ila falsafa za uongozi na uchumi haziwezi.
 
Waotaji oteni tu. Ninachojua ni hivi, hata zikipigwa kula leo hatapa ushindi chini 80%, trust me, wapiga kura wa ccm ambao wengio siyo wasomi wala hawaishi mijini kwenu, watampa kura nyingi sana hata mimi nikiwemo.
 
😡😡😡😡😡😡😡
 
Amefanya mazuri yapi?

 
CCM hawafanyi tena mchakato wa kumpata Mgombea mwingine mpaka aliyepo amalize miaka 10 kwenye enzi.
Na huo mchakato maana yake kutakua na mwenyekiti mwingine wa chama wa muda..it meanz watampindua embu kuweni serious kidgo yule ndo president na ndo chairman wa CCM..nan anabisha..[emoji34][emoji34][emoji34]
 
Bana Paskali ndo wewe wa kule kwenye uzi wa Juma Pinto ukitokea na @Pasco?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…