Mwesiga frolian
Member
- May 9, 2023
- 18
- 14
UTANGULIZI
Kama ilivyo kwa vijana wengi wa kitanzania nilikuwa na ndoto ya kumaliza shule kwa kutaka kusoma kadri ya uwezo wangu ili mwishowe niweze kuhitimu masomo yangu, nipate kazi ambayo ingenisaidia kujikimu na kuinua kipato changu pamoja na kusaidia familia yangu kuondokana na wimbi la umaskini. Nilikuwa ni mtu anayependa kusoma ili niwe na mawazo mapana , hakuna ambacho sikupenda kusoma ila changamoto za kimaisha zilikatisha ndoto yangu ya kumaliza shule jambo ambalo lilinifanya niwe nafika shuleni nimechoka sana, nachelewa kila wakati muda mwingine kuadhibiwa kutokana na kuchelewa.
Changamoto hizi zilizokatisha ndoto yangu ya kumaliza shule zimenisukuma kuandaa andiko hili lenye kuchochea mabadiliko chanya kuhusu uwajibikaji na utawala bora katika sekta ya elimu kwa kuainisha changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi yakinifu.
Changamoto ya kifedha; Licha ya serikali kufanya jitihada za kuondoa ada katika elimu kuanzia ngazi ya msingi mpaka kidato cha sita bado changamoto ya kifedha ni kikwazo katika sekta ya elimu. Wanafunzi wengi bado hawana uwezo wa kwenda shuleni kwa sababu nyingine za kielimu, wazazi walezi hawana uwezo wa kuwalipia nauli ya kwenda shuleni, kununua sare na mahitaji mengine kama vitabu. Endapo shule zinakuwa mbali wanafunzi hulazimika kupanga hosteli binafsi ambapo familia nyingi maskini haziwezi kumudu suala hili.
Ubora wa elimu unaotolewa upo chini ya kiwango; kwa mjibu wa ripoti ya Benki ya Dunia juu ya viashiria vya utoaji huduma katika mnyororo wa matokeo ya elimu ( WBI SDI report of 2016) idadi kubwa ya walimu bado hawana stadi za kitaaluma na uelimishaji zinazohitajika ili kufundisha ipasavyo hivyo kupelekea ubora wa elimu kupungua. Pia kutokana na changamoto ya ukosefu wa walimu katika baadhi ya masomo hususani sayansi na hesabu wanafunzi wengi huendelea na masomo bila walimu wa masomo haya kwa kipindi cha muda mrefu na wakati mwingine kutafuta njia mbadala kwa kulipia mafunzo binafsi ya ziada ambapo sio wote wenye uwezo wa kulipia jambo ambalo hupelekea wanafunzi wengi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao.
Mtihani wa kitaifa kwa shule za msingi unazuia upatikanaji wa elimu; vijana wengi nchini Tanzania wameshindwa kupata elimu ya sekondari baada ya kushindwa kufaulu mtihani huo wa darasa la saba ambapo serikali huruhusu wanafunzi waliofaulu tu kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari na hakuna mwanya au nafasi ya kurudia mtihani huo. Mfano Tangia mwaka 2015 mpaka 2022 Vijana milioni 1.6 wapo mtaani kwa kushindwa kujiunga na elimu ya sekondari.
Changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia; kumekuwepo na kasumba isiyoisha ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike pamoja na wanafunzi wa kiume kutoka kwa walimu wao, madereva wa mabasi ya shule, watu wazima, bodaboda ambao hutaka ngono kwa kuwapa zawadi, lifti au pesa wakati wakiwa njiani kuelekea shule. Mfano baadhi ya shule nyingi hushindwa kutoa taarifa za unyanyasaji huu kwa vyombo vya kisheria jambo ambalo linakatisha ndoto za vijana wengi kuendelea na masomo yao.
Changamoto ya miundombinu; Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali ( C.A.G) iliyotolewa Mwezi mei 2023 inaonyesha halmashauri 45 nchini Tanzania zina upungufu wa madawati 150,066, matundu ya vyoo 56,550, vyumba vya walimu 35,664, na upungufu wa madarasa 27,316, uhaba wa walimu 100,958 ya shule za msingi, sekondari walimu 74,743 sawa na asilimia 47. Pia ndoto za wanafunzi wengi huishia njiani kwa kushindwa kumaliza shule kutokana na changamoto ya miundombinu mibaya na ukosefu wa usafiri mashuleni .wanafunzi wengi wa kijijini wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda shule, jambo linalofanya wanafunzi kufika shuleni wakiwa wamechoka sana hivyo kuathiri mfumo wao wa kujifunza, walimu pia hawakidhi idadi ya wanafunzi waliopo shuleni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishia.
NINI KIFANYIKE ILI VIJANA WAWEZE KUTIMIZA NDOTO YAO YA KUMALIZA SHULE?
Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kupitia ibara ya 8(1),(c) imeelezea bayana kwamba serikali inapaswa kuwajibika kwa raia wake. Pia kupitia ibara ya 11(2), (3) inasema kwamba kila mtu ana haki ya kupata elimu.
Suluhisho la changamoto hizi ni uwajibikaji pamoja na uongozi imara katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha kwamba kunakuwepo na ufumbuzi wa changamoto hizi kwa kuhakikisha kwamba kuna mkazo katika kupanua wigo na upatikanaji wa elimu, pia kuhakikisha ubora wa elimu inayotolewa ni kwa wanafunzi wote, kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanawezeshwa kwa kupatiwa ujuzi na kujenga maarifa maalum ili kupeleka Tanzania mbele.
Imeandaliwa na mwesiga frolian.- lawyer.

Upvote
5