Ukiota mazingira ya shule, upo na ma classmates wa siku nyingi zilizopita, mfano unaota upo katika mazingira ya shule yako ya msingi na upo na wanafunzi mliosoma nao wakati ule pengine imepita miaka mingi inamaanisha kwamba kuna kitu cha kiroho kinachoendelea katika maisha yako kinachohusiana na mambo ya siku zilizopita.
Chunguza maisha yako vizuri unakuta kuna mambo haya yafuatayo:
- umekuwa ukikwama katika mambo yako kila wakati
- unaishi nyuma ya wakati wako; yaani ulipaswa kuwa mbali zaidi ya hapo ulipo
- huridhiki na maendeleo yako pamoja na kuwa na elimu kubwa na ujunzi mzuri
- ulikuwa unafanya vizuri darasani lakini maendeleo yako sasa hayalingani na kipaji chako
- umekuwa na ambitions za kitaaluma lakini hujaweza kuzifikia
Kuota ndoto za shuleni mara kwa mara kwaweza kumaanisha kwamba bado hujatenganishwa na wakati uliopita, na umekwamishwa kiroho kuvuka na kwenda kwenye nafasi yako ya ukubwa au mafanikio.
Hivyo basi unapaswa kuchunguza maisha yako. Angalia historia ya familia yako, baba, mama, kaka na dada zako, je nao wapo kwenye hali ya kuchelewa maishani?
Unahitaji kuondolewa hapo ulipokwama kiroho kabla hujachelewa mno. Inategemea imani yako ilivyo lakini haijalishi pia, kwani Mungu huongea kila wakati na kila mtu kwa namna yake ikiwa ni pamoja na kupitia ndoto. Ila tatizo ni kwamba wengi wetu hatutambui kabisa kwamba Mungu amezungumza licha ya kutambua amezungumza nini!
Unahitaji kutoka hapo ulipo kiroho, umekwama au umekwamishwa kiroho. Ulimwengu wa kiroho upo na unafanya kazi kwa ufanisi na usahihi usioelezeka. Tafuta watu ambao kweli ni watumishi wa Mungu Mwenyezi na uwaeleze shida yako nao watakuombea na kukusaidia '"Kutoka" hapo ulipo. Nawe kuanzia sasa anza kuzungumza na Mungu kama unavyozungumza na yule unayemheshimu sana, mwambie kila kitu, kila shida yako na mwombe specifically unachotaka akufanyie ukitaja tatizo lako barabara na kumwambia unataka afanye nini hasa. Fanya hivyo bila kuchoka ama kuona aibu kila wakati. Fuatilia matokeo yake na pia andika uombacho na tarehe, fuatilia maombi yako kwa imani, Mungu si mwanadamu ili asahau au ashindwe kukujibu, atakujibu tu, kuwa mwangalifu akizungumza umsikie kwani ndipo tatizo kubwa la mwanadamu; wengi hawasikii Mungu anapozungumza! Atazungumza na kukujibu kila kitu, fuatilia kwa uangalifu mkubwa, Mungu ni mwaminifu mno na hujibu kila ombi!
Kama una maswali zaidi nitakusaidia zaidi, tuwasiliane. Nimekuwa katika hali kama hii naifahamu vizuri na ninaendelea kutoka kwa kasi kubwa kila siku.