Ndoto ya kuwa Pilot jamani

Ndoto ya kuwa Pilot jamani

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,188
Reaction score
6,244
Habari zenu wakuu. Mwenzenu apa nna ndoto za kuwa airline Pilot japo tanzania hatujawa na kampuni zenye kumiliki boeing na airbus (itoe fastjet mana si yetu). Tatizo kipato kinanizuia maana cost za kusomea zinafika ama kupita milioni 100. Sasa nlikuwa na wazo la kupitia jeshini ili nipate mafunzo ya urubani. Naombeni munipe taratibu inakuaje mpaka unakuwa admitted katika kikosi cha anga. Mikiki ya jeshini itanitesa kwani na ka pumu kananisumbuaga kwenye kazi nzito. (Pumu haimzuii mtu kuwa pilot)
 
si lazima uende jeshini kuna njia mbadala unaweza kutumia kwa gharama nafuu,ieleweke kwamba urubani huenda ngazi kwa ngazi,hatua moja hadi nyingine kama ifuatavyo........
 
1.lazima kwanza upate spl-student pilot licence
 
Subiria subiria nilisikia kuwa NIT wana mpango wa kuanzisha mafunzo ya urubani..

Lini na ngazi ipi hilo mimi sijui...
 
ukishapata no.4 ki msingi utaruhusiwa kurusha (big boys),mipipa mikubwa kama ndoto yako inavyotaka la muhimu hapa tafuta flying school za kawaida hapa hapa bongo kwa ajili ya namba 1. kuanzia namba mbili utaingia mikataba na makampuni popote pale ambao utakuwa unafanya kazi kwao na huku unachanga masaa ktk log book yako,then kuanzia hapo inakuwa rahisi kupata mfadhili kwa ajili ya kusomea aina ya ndege unayotaka kuirusha.kitu ambacho hutakisahau ktk maisha yako ya urubani ni the second effect of control hii ukipass wewe lazima utakuwa rubani tu.
 
5h-ndege zilizosajiliwa tz
5y-ndege zilizosajiliwa ky
5x-ndege zilizosajiliwa ug
 
Nani kakuambia bongo ndoto za watu huwa zinatimia?we jiandae kuwa mwalimu tu,hakuna cha pilot wala nini!
 
Subiria subiria nilisikia kuwa NIT wana mpango wa kuanzisha mafunzo ya urubani..

Lini na ngazi ipi hilo mimi sijui...

Asante mkuu, ila quality sijui itakuaje Tanzania yetu unaijua tena, airliners wanatizama nao leseni umeipatia wapi?
 
4.air transport pilot licence

Nzalendo nakushukuru kwa response yako, lakini kama nlivosema mwanzo, kipato ni ishu, kwa level ya PPL ni dola elfu 15, hapo sio pafupi ndugu yangu. Umezungumza kuhusu kupata kampuni ikakufadhili kwa hatua ya pili, tanzania nani anafanya iyo kitu? Precision wenyewe naskia waliwaambia watu wakajisomeshe ratings ya ATR42 kwa pesa zao.
 
kama usipokutana na wachawi wa kuuwa ndoto za watu lazima zitatimia

Mkuu watu wa design hii mi hawanitishi kabisa, eti alikuwa na ndoto za kuwa rais blah blah, kama yeye hana mipango ya kuupata urais ataishia kuota tu ata kujaribu hatoweza. Ishu ni kuwa determined, ndio maana hawa majamaa hawaendi mbele, nawapa pole sana!
 
Usikate tamaa dogo, unaweza kufanikisha ndoto zako ikiwa tu, hutokata tamaa... kuna wengi tu ambao wametimiza ndoto zao ndani ya Tanzania hii hii... taratibu utafika.
 
Usikate tamaa dogo, unaweza kufanikisha ndoto zako ikiwa tu, hutokata tamaa... kuna wengi tu ambao wametimiza ndoto zao ndani ya Tanzania hii hii... taratibu utafika.

Asante dada, mi si mtu wa kukata tamaa nashkuru, i believe in what i want, na nnta fight for it, atleast at the end, ntakuwa nimetumia some effort kuliko kukaa tu bila ya kufight! Asante
 
Back
Top Bottom