SoC02 Ndoto ya mafanikio

SoC02 Ndoto ya mafanikio

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 28, 2022
Posts
7
Reaction score
4
Maisha ya wanadamu hupangwa na Mungu ila kijituma na kutokata tamaa ndo msingi wa mafanikio kwa mwanadamu, Katika kijiji kimoja alikuweko kijana aliyeitwa Amour, Amour alikuwa na umri wa miaka 15, KIjana huyu hakuwa na elimu ya darasani lakini Mungu alimbariki Hekima, Ucheshi na Busara kwa kila mmoja, Kiukweli alitamani sana naye angepatiwa elimu ila kwa hali ya umaskini wa familia yake ilishindikana kununuliwa hata sare za shule.

Kutokana na umaskini huo Amour aliqnzisha kilimo cha mboga mboga huku akilini mwake akiwa qnaupinga ule usemi wa wahenga usemao "Mtoto wa nyoka ni nyoka" ,Siku zote aliamini kwamba ipo siku atarudi shule nag kuikomboa familia yake kutoka katika umaskini wa kutupa,Siku zilizidi kwenda huku akiwa anajishughulisha na kilimo ambacho kilikidhi mahitaji yao madogo madogo katika familia.

Kwa hali ya umaskini wa nyumbani kwao Amour bado aliishi katika ndoto yake ya kusoma na kuwa kiongozi mwanamapinduzi katika nchi yake,Lakini alibaki na maswali kwamba itawezekanaje ndoto yake kutimia?

Siku moja alipata mteja kutoka mjini ambaye alihitaji mafungu ya mboga za majani yapatayo 150 ,Amour bila ya kuchelewa alianda Gari mpaka mjini akiwa amevalia kandambili nyekundu mguu wa kulia na nyeusi mguu wa kushoto,fulana ya njano na Bukta ya bluu zilizokuwa chakavu sana.

Alifanikiwa kufika mjini ikiwa ni saa 6 mchana , Bila kuchelewa alibeba gunia lake la mboga mgongoni huku akiwa anatembea kwa kuinama, Mbele kidogo alipoona kijana akipita na mzazi wake wakiwa wametoka shule alichelewa kustahimili machozi muda mchache akafuta machozi kwa mkono wake wakulia.

Akawa amesimama pembeni mwa barabara kwa ajili ya kuvuka kwenda upande wa pili, ghafla ikatokea gari ubavuni mwake ambayo ambayo ilikosea muelekeo na ikamgonga, kijana Amour alipoteza fahamu hapo hapo, Yule dereva akashuka na kumbeba kumkimbuza hospitali kubwa ya mkoa,Madaktari walimsaidia Amour kwa kipindi kigumu walimsaidia Amour kwa kipindi kigumu alichokua anapitia lakini ilishinjdikana kurudisha fahamu yake kwa haraka, Pindi Amour akiwa katia usingizi mzito wa kukata fahamu akawa anaota "Wananchi Oye! Oye! Wananchi Hai!, Hoi! " Alisema amour usingizini wananchi waliitika Hai! Bila kupoteza muda napenda kusema asante kwa kila mwananchi na mwanachama wa chama cha WAPENDA MAENDELEO (CWM) kwa kunipa kibali cha kuongoza nchi hii ya PARIBUS,Bila kusahau kipaumbele changu ni ELIMU KWA WOTE.Basi shangwe,vifijo na ndelwmo vilitawala kila kona ya nchi hiyo.

Baada ya hiyo ndoto kupita ghafla Amour alishtuka akiwa anahema sana,Alipofumbua macho alikutana na Baba yake huku yule kijana dereva akiwa pembeni yake akiwa haamini kilichotokea. Kiukweli alilia kwa uchungu sana Amour huku kuilio chake kikiambatana na kwikwi isiyokoma,Baada ya wiki mbili Amour aliruhusiwa ila yule kijana baada ya kuongea na Amour na kujua malengo na ndoto zake alijitolea kuwa mdhamini wake wakimasomo, Amour alipata nafasi ya kusoma shule ya kuanza kidato cha kwanza (kwani alimaliza elimu ya rasaba kijijini kwao) katika shule ya "TUKUMBUKANE" Na elimu yake yajuu(Advance) katika shule ya wavulana "MAPAMBANO" , Mungu hakumtupa mkono alifanikiwa kumaliza elimu ya chuo na kutunukiwa PHD katika Elimu.

Alirudi nyumbani akiwa na furaha sana kwakuwa ndoto yake ilitimia hata wazazi wake walifurahi sana ,Mungu si Athumani haikupita muda Amour akafiwa na mama yake kwa ugonjwa wa kansa ya koo uliomsumbua kwa muda sana ,Majonzi na Simanzi vilitawala lakini haikua mwisho wa safari ya Amour.

Akiwa na miaka 43 Amour aligombea nafasi ya uraisi na kupita kwa kishindo, Siku hiyo Amour alishindwa kujizuia kutoka machozi mbele ya kadamnasi baada ya kutajwa yeye kuwa yeye ndiye mshindi wa kiti cha uraisi alipiga magoti na kunyanyua mikono juu akisema " Mungu hajawahi kumuacha mja wake na Elimu ndo mkombozi na mtatuzi wa kila litalajiwaloAlijikaza kama mwanaume akalihutubia Taifa na mwisho alisema "KUJITUMA,HESHIMA,HEKIMANA KUTOKATA TAMAA NA ELIMU, YOTE PAMOJA YAKIUNGANISHWA HAKUNA KITAKACHOSHINDIKANA" Shangwe na ndelwmo baada ya maneno hayo kukonga nyoyo za wananchi

Raisi Amour alihakikisha watoto wotewanaoishi katika mazingira magumu nchini wanarudi shule na kutoa ada kwa shule za msingi hadibelimu ya juu kiukweli watu wengi walimpenda ujali wake kwa watu wote wenye hali ya chini kimaisha.

Haikuishia hapo alifanya juudi kujenga mabweni kwaajili ya wanafunzi wa kike kuwaepusha na kupata mimba zisizotarajiwa kwa kutembea umbali mrefu na kurubuniwa na waendesha bodaboda.

Mwangaza ulionekana kuonekana nchini pote na ujinga ulianza kupungua katika vichwa vya watu baadhi ya watu walianza kuruhusu watoto wao wakike kwenda shule,Jamii ilizinduka kutoka katika kiza kilichotawala fikra zao.

Amour ni mwanamapinduzi kupitia sekta ya Elimu aliyoipigania kwa muda mrefu kuipata pia akawa na mfano wa kuigwa nnchini na nchi jirani katika kila sekta iliyohusu Elimu hakuwa mchoyo kushauri maraisi wenzake katika umuhimu wa kumpa mtoto Elimu ya darasani hata ya kujitambua.

Kila kona ya dunia zilienea sifa zake kwa mema yake na nuru aliyoitengeneza,Kila aliyesikia historia ya maisha yake na jinsi gani elimu ilivyomkomboa ilisaidia kw avijana waliokata tamaa.

Alishika mshikani wake hadi mwisho wa utawala wake,Alifanikiwa kuchapisha kitabu kiitwacho "MAISHA YANGU " Kitabu hiki kilitumika kama chachu kwanzia nchini hadi nje ya nchi.
 
Upvote 2
Kali Sana
giphy.gif
 
Back
Top Bottom