Ndoto ya mbwa mwitu

Ndoto ya mbwa mwitu

RoadLofa

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,509
Reaction score
3,313
Nimeota tumeenda nyikani mi na rafiki yangu mmoja ambaye simkumbuki vizuri ila nakumbuka kama alikuja kunipitia ninapokaa

Tukaenda porini/nyikani mbali kidogo na tunapoishi mara tukawaona sungura tukavutiwa kuwakamata na tukaanza kuwafuatilia

Ili tuwakamate,ghafla tukamuona mbwa mwitu kwa mbali anakuja mwelekeo wa kijiji tunakoishi na ndio tulikotoka

Tukaanza kukimbia ili kumuwahi yule mbwa mwitu kabla hajafika kijijini ili kuwastua wanakijiji wenzetu kujilinda ili wasizulike na yule mbwa mwitu tuliprofika karibu na kijiji tulikuwa tunapiga kelele nyingi za kuwaambia pandeni juu ya miti ,pandeni juu ya miti mbwa mwitu anakuja ,wachache walielewa chap walipanda wengine walikuwa wazito kuelewa mapema

Mbwa mwitu alipotukalibia tulikuwa tushafika kijijini mi nililukia juu ya mti na watu wengine walinifuata kwenye mti

Niliopanda wakapanda matawi mengine hadi yakaelemewa na mbwa mwitu alikuwa ameshafika na kuanza kushambulia watu ndipo wanakijiji wakajitoa muhanga kupambana naye kwa silaha na wengine wakiwa bila silaha,katika kupambana na uyo mbwa mwitu

Kuna jamaa namkumbuka kwa sura kama ali nilikuwa nasoma naye primary yeye akajitoa muhanga akampiga roba ya mkono mbwa mwitu

Kitu kilichopelekea ali kushabuliwa sana kichwani na mbwa mwitu ila akumuacha mbwa mwitu,nilivyomwangalia ali kichwani

Nililia sana ila ali alifariki pale pale akiwa shingoni mwa mbwa mwitu na mbwa mwitu akiwa amekufa
msiba wa ali watu walijaa sana kwa sababu ni shujaa na mi nilikuwepo nililia sana.

Iyo ndoto ina maanisha nini wakuu?
 
Back
Top Bottom