Costancia Adauthy
Member
- Apr 19, 2024
- 7
- 4
Utangulizi
Elimu ni nyenzo pekee ya kujenga ujuzi, maarifa, uwezo wa kupambanua mambo, udadisi na kujiamini ambako huchochea mapinduzi ya fikra, hatimaye maendeleo ya jamii husika.
Changamoto ya elimu ya sasa
Mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yameibua kasoro kwenye elimu yetu kama ifuatavyo
a;Sera ya elimu inayokidhi mahitaji ya jamii ikiwashirikisha wasomi, wadau, tafiti za elimu, taasisi na wanajamii ili kukidhi mahitaji ya sasa na baadae na kulinda tamaduni zetu, kwa vipaumbele vifuatavyo
b; Uanzishwaji maktaba kidijitali ( digital library) chini ya mwamvuli wa maktaba ya taifa.
LENGO
mfano wa maktaba ya kidijitali. Source: google
g; sheria za utunzi na uandikaji wa vitabu vya masomo, kiada (textbook)na ziada.(supplimentary book), ili kukwepa makosa ya kimuundo na kimaana. Mambo ya kuzingatia
h; Uwepo wa stesheni ya redio na luninga yenye maudhui ya kitaaluma.kwa kufanya yafuatayo
i; Utungwaji wa sheria ya uanzishwaji vituo vya elimu kwa wasichana walioshindwa kuendelea na masomo kwa kupata ujauzito na sababu nyingine. Kwa kuzingatia yafuatayo
Hitimisho
Vipaumbele hivi vinabebwa na uwajibikaji kwa wote,bajeti yenye kukidhi mahitaji ya elimu na uwepo wa viongozi wenye maono. Mwanamajumui amemalizia.

- Uhaba wa miundombinu, madarasa, walimu kwenye masomo yote ukilinganisha na uwiano wa wanafunzi, maabara, vitabu, vyumba vya kompyuta, maktaba za shule, ukosefu wa vifaa vya kufundishia, kwa vitendo, ambako hupelekea
- Uwasilishwaji duni wa somo, mfano somo la kingereza kufundishwa kwa kiswahili hasa shule za msingi.Ujifunzaji chini ya kiwango na Utathiminishaji usio na usawa hasa kwa shule zenye uhaba wa miundo mbinu na shule zilizo na utoshelevu.
- Wahitimu waliokosa ubora kimataifa. Wahitimu kuibukia katika elimu iliyo nje ya mfumo ambayo hawana ujuzi na kuzalisha chini ya kiwango
- Kupungua kwa hari ya vijana kusoma kwa kuhofia kupoteza muda shuleni na kukosa ajira
- Kuongezeka kwa michezo ya kubahatisha.
a;Sera ya elimu inayokidhi mahitaji ya jamii ikiwashirikisha wasomi, wadau, tafiti za elimu, taasisi na wanajamii ili kukidhi mahitaji ya sasa na baadae na kulinda tamaduni zetu, kwa vipaumbele vifuatavyo
- Mipango ya elimu iwe jumuishi, isiandaliwe na wanasiasa tu bali ihusishe wasomi na wadau kada ya elimu
- Mitaala yenye kubainisha njia bora za ufundishaji na kuweka kipaumbele matumizi ya tehama, elimu ya vitendo, kazi za vikundi, utafiti mada na uwasilishwaji.
- Kingereza kua lugha ya kufundishia,
- Wanafunzi kusoma masomo ya fani zao kwa shule za sekondari.
- Uzalishaji na uwezeshwaji walimu kwenye masomo ya sayansi, hisabati, tehama, English na masomo mapya.
- Kuboresha mfumo wa upimaji na Utathiminishaji, kuondoa njia ya kusiliba kwenye somo la hesabu shule za msingi na kutumia njia ya kukokotoa hesabu
b; Uanzishwaji maktaba kidijitali ( digital library) chini ya mwamvuli wa maktaba ya taifa.
LENGO
- Kurahisisha upatikanaji wa vitabu vya ziada na kiada kwa masomo ya masafa kwa kuhakikisha,
mfano wa maktaba ya kidijitali. Source: google
- Ugawaji wa kompyuta na vishikwambi ili kuwawezesha wanafunzi kuperuzi mtandaoni kwa uwiano sawa na idadi ya wanafunzi.
- Kuruhusu matumizi ya mnara mmoja wenye nguvu kwa mitandao yote hasa maneo yenye changamoto ya mtandao.
- Uwepo wa program ya kuhifadhi (offline)baada ya kupakua.
- Gawio la faida kwa waandishi na wasomi watakaoweka kazi zao.
- Kutenga bajeti kwa maprofesa wa vyuo vikuu ili kuwapa hari ya uwezeshaji elimu kwa kufanya tafiti za elimu
- Kusapoti mihadhara ya kiprofesa na kuwapa hari vijana kuhudhuria, kufuatilia mihadhara na machapisho
- Ufadhiri wa masomo na kiuchumi wahadhiri walio ngazi ya chini mfano wa shahada ya uzamili.
- Kuondoa kigezo cha ufaulu wa juu bila kuangalia uwezo wa ufundishaji, kuwa kipaumbele cha ukufunzi.
- Uwepo wakanuni na taratibu zitakazompa kuwajibika mwanafunzi na msimamizi kwenye taasisi.
- Kuongezeka kwa muda wa mafunzo kwa kada za sayansi na teknolojia ya ubunifu
- Ongezeko la fedha za kujikimu za field kutoka bodi ya mikopo ili kuwezesha
- field za kimataifa, hasa masomo ya sayansi na teknolojia.
- Kuajiri wakufunzi toka nchi zilibobea kidijitali,
- kualika wataalam bobezi wa nje na ndani kutoa mihadhara
- Kufufuliwa kwa shule kongwe za kilimo
- Uwepo wa karakana ya kidijitali.
- Ufadhili wa wanafunzi wa kada ya kilimo kwa asilimia mia moja, na kuwapa fursa ya ziara katika nchi zilizobobea katika kilimo cha kidijitali.
- Kuanzishwa kwa mtandao utakaochapisha ubunifu za kilimo.
- Sanaa(Arts) ikijumuisha sanaa ya uchoraji (Fine art) mziki, michezo ya viungo kukimbia, kuruka viunzi, ngoma na maigizo
- Fasihi ya lugha. Fasihi ya kiswahili na kingereza, hususani uandishi riwaya tamthiria, utenzi na hadithi za watoto.
- Stadi za nyumbani(home economics) sanaa ya mapishi(cookery) sanaa ya ushonaji(needle work)
g; sheria za utunzi na uandikaji wa vitabu vya masomo, kiada (textbook)na ziada.(supplimentary book), ili kukwepa makosa ya kimuundo na kimaana. Mambo ya kuzingatia
- Vitabu viandaliwe na wabobezi wa fani au somo husika, na kuhakikiwa na taasisi husika
- Vitabu vya lugha, mfano kiswahili, kingereza nk, viandaliwe na wabobezi wa lugha husika, na kuhakikiwa na mabaraza
- Tafiti zifanyike kugundua mahitaji ya elimu.
- Kuzuia kutumika kitaaluma vitabu visivyohakikiwa
h; Uwepo wa stesheni ya redio na luninga yenye maudhui ya kitaaluma.kwa kufanya yafuatayo
- Serikali na taasisi za elimu kuidhamini
- Umataifashaji( internationalization) wa elimu kwa njia ya mtandao kufundishwa na walimu wa kimataifa
- Kuwapa nafasi walimu wazalendo kufundisha mada na kuwapa motisha
i; Utungwaji wa sheria ya uanzishwaji vituo vya elimu kwa wasichana walioshindwa kuendelea na masomo kwa kupata ujauzito na sababu nyingine. Kwa kuzingatia yafuatayo
- Vituo vya elimu nje ya shule zao za awali.
- Halmashauri ihakikishe serikali za mitaa zinaandaa madarasa katika muda wa jioni
- Asasi za kijamii zitoe elimu ya ujinsia, kujilinda na ujauzito tena, elimu ya ujasiliamali ili kujikimu kimaisha.
Hitimisho
Vipaumbele hivi vinabebwa na uwajibikaji kwa wote,bajeti yenye kukidhi mahitaji ya elimu na uwepo wa viongozi wenye maono. Mwanamajumui amemalizia.
Upvote
3