Elections 2010 Ndoto yangu 2015: Dr slaa awe rais na mtikila waziri mkuu

Elections 2010 Ndoto yangu 2015: Dr slaa awe rais na mtikila waziri mkuu

mzambia

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
885
Reaction score
60
Jamani katika hali ya kushangaza leo nimeota ndoto dr slaa kawa rais 2015 afu kamteua rev mtikila kuwa waziri mkuu, afu mwakyembe waziri wa sheria, magufuli waziri wa maadili na utawala bora, zitto kabwe waziri wa nishati na madini, john mnyika waziri wa habari na michezo, pinda katibu mkuu kiongozi,
tibaijuka makazi na mazingira, prof luhanga elimu. Hakuna naibu waziri na wizara zingine nimezisahau.

Kama kuna mwenye mawazo pls
 
Njozi....watanzania hawamtaki huyo mtu..mpeleke akawe rais nyumbani kwako.
 
Jamani tusidharau maana kipindi kile kina nostradamus wanatabiri kupitia ndoto watu walidharau sasa yanatokea wanashangaa
 
mie nathani uote tena halafu Wizara ya katiba na sheria iwe chini ya Mtikila au Mwakyembe! Waziri Mkuu awe Magufuli au Tibaijuka
 
Sijakupinga popote. Ila ukiota tena ili tundu lissu awemo itakuwa imekaa poa.
 
Tundu lissu wizara ya sheria na katiba
afu mtikila wizara ya viwanda na biashara ili awatimue ma*********
 
Weeklickage imesema Tanzania hakuna uchaguzi 2015 ! Kwani hata hao uliowataja umri wao hauwaruhusu kuwa raisi tayari vimeshakuwa vizere.
 
Tundu lissu wizara ya sheria na katiba
afu mtikila wizara ya viwanda na biashara ili awatimue ma*********

Kwa heshima ya Rev. Mtikila, hiyo wizara ya viwanda na biashara iunganishwe na ile ya makazi ili kumpa uwanja mpana zaidi mtikila wa kufanya kazi
 
Mwakyembe HAFAI kufanya kazi zilizo karibu na Wananchi wasio wasomi.

Huyu anafaa zaidi kwenye maeneo kama East Africa Parlament, SADC, uandishi wa mikataba nk......

Uwezo wake mkubwa sana na anatumika vibaya. Hana KIPAJI cha kufanyakazi na Wasio wasomi.
 
Mkuu Sikonge nimekupata vilivyo na uko sahihi
Kweli tuna watu wazuri tunawatumia mahala pasipokuwa kwao na hivyo kufanya wakati mwingine washindwe kufanya kila kinachotarajiwa
 
Jamani katika hali ya kushangaza leo nimeota ndoto dr slaa kawa rais 2015 afu kamteua rev mtikila kuwa waziri mkuu, afu mwakyembe waziri wa sheria, magufuli waziri wa maadili na utawala bora, zitto kabwe waziri wa nishati na madini, john mnyika waziri wa habari na michezo, pinda katibu mkuu kiongozi,
tibaijuka makazi na mazingira, prof luhanga elimu. Hakuna naibu waziri na wizara zingine nimezisahau.

Kama kuna mwenye mawazo pls

Nchi gani hiyo???? Mtikila haitambui Tanzania anaitambua Tanganyika ndoto yako ime Skip ilitakiwa ianze kwa kuvunjika Muungano, kukamatwa kwa Zitto na Kafulila
 
Mnyika Habari??????????hapana,Kazi ajira na Maendeleo ya Vijana atusaidie na suala la baraza la vijana linalopigwa chenga kila siku hiyo ya Habari apewe hata Suzan Lyimo........Regia wangu mumpe ya wanawake,watoto na maendeleo ya jamii na Halima Mdee apewe hiyo ya Sheria na Katiba,Tundu Lissu apewe maadili na utawala bora............please naomba uote tena..........LOL
 
mie ni muumini sana wa ndoto na hasa ninapowasoma watumishi wengi katika vitabu vya dini.
sasa kama sio ndoto za shibe hasa wakati huu wa sikukuu mfururizo basi upo sahihi 100% kwenye
suala la Mheshimiwa Dr.Slaa kuwa Rais tena kwani hata awamu hii yeye ndiye alikuwa Rais ila
UGHIBAGHIBO ndio uliotumika hapo.
DR.SLAA ni mtu wa Mungu hakutaka waitwe Marais wa EA kuleta suluhisho kwa kutaka
kung'ang'ania kwenda IKULU,tuatwaona hao waliong'ang'ania kwenda jinsi WIKILEAKS
inavyowaumbuwa kwanza halafu 2015 watujibu vizuri shutuma zao.
 
Ukiota Makamba makamu wa Rais, nenda Bagamoyo wakakuague mlingotine maana huo utakuwa ni uchuro na mwaka huu utakuendea vibaya. tehe tehe!
 
Back
Top Bottom