SoC02 Ndoto yangu ilivyosimama

Stories of Change - 2022 Competition

Perpe

Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
5
Reaction score
2
(Hii makala ni kisa cha kweli kilichotokea maishani mwangu)

Nilikuwa nikitamani sana kuwa daktari wa magonjwa ya moyo,tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikijihamasisha kwa kusoma kwa bidii ili siku moja niwe daktari mwenye msaada mkubwa kwa nchi yangu,Mungu alinijalia uelewa mkubwa darasani na juhudi hivyo nilikuwa nikifanya vizuri.

Nilipofika darasa la sita nikapata tatizo la kutosikia vizuri, nilihangaika hospitali lakini sikupata suluhisho la kudumu,tatzo lile lilipelekea hata darasani kutomsikia vizuri mwalimu lakini sikukata tamaa nkazidisha bidii kwa kujisomea mwenywe hatimaye nkamaliza elimu ya msingi na kufaulu kwa alama za juu kwenda sekondari.

Nilichukua masomo ya sayansi ikiwa kama njia ya kufikia ndoto yangu, japo nilipata changamoto kuelewa darasani kutokana na tatizo langu lakini nilizidi kupambana, nlidunduliza hela za shule kununua vitabu vya kila somo ili niwe najisomea zaidi maana kwangu mimi ndo nlikuwa mwalimu na mwanafunzi, juhudi hazimtupi mtu nkafanikiwa kuhitimu kidato cha nne na kufaulu kwa daraja la kwanza na hatimaye kujiunga kidato cha sita

Nikachukua mchepuo wa sayansi wa PCB darasa haswa kwa ajili ya kuwaandaa madaktari wa baadae, lilikuwa darasa gumu hasa kwa hali yangu ya kutosikia vizuri lakini Mama yangu alinipa moyo kila siku kwamba juhudi hazimtupi mtu na nitafikia ndoto yangu kwani nchi yangu ni nchi ya amani na nitawezeshwa.

Nikafanikiwa kumaliza kidato cha sita, nikafaulu kwa daraja la kwanza na kuchaguliwa kwenda chuo kusomea shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu, nililia na kumshukuru Mungu kufika pale na kumwomba anipe nguvu za kuendelea, hatimaye nikaripoti chuo,nikawataarifu uongozi kuhusu hali yangu na wakanipa moyo na kuniahidi kunishika mkono nitakapokwama.

Nikaanza masomo na kufanikiwa kumaliza miaka miwili ya mwanzo vyema kwa bidii japo haikuwa rahisi,nikaingia mwaka wa tatu, mwaka ambao ndoto yangu ilianza kusuasua,tuliingia mwaka wa vitendo zaidi na kusoma kwa mafunzo ya hospitali,kuonana na wagonjwa na kufanya mitihani, ilikua ngumu kwangu mno nilijitahidi kupambana na kusogea mpaka nusu mwaka, lakini nikaonekana siwezi.
Niliomba sapoti kutoka chuo lakini haikusaidia kubadilisha maoni ya walimu wengi kwamba haiwezekani mtu wa hali yangu kusomea kitu kama udaktari, nikaitishiwa kikao na kutakiwa kuacha kuendelea kusoma.

Nilichanganyikiwa na kuathirika mno kisaikolojia, kila siku nilikua mtu wa kulia, juhudi zangu zote nikiwa bado nna miaka miwili kufikia ndoto yangu leo hii niiache?
Nilipambana mpaka taasisi za juu kuomba msaada ili niweze kuendelea kusoma nikiamni kwamba hata walemavu wakiwezeshwa wanaweza lakini nilizidi kuumizwa, kuna walionipa tumain la muda mfupi na kuniacha njiani, kuna walioniumiza kwa kuniambia ungekuwa mzima kabisa isingekuwa shida
Nilipambana na kujaribu kuhama mpaka chuo lakini ikashindikana

Nikakata tamaa na kurudi nyumbani, wenzangu wakamaliza mwaka wa tatu, nlikuwa mtu wa huzuni,mawazo, kuna muda nilitamani kujiua,nilijichukia kwa kuwa nikaona kama mimi kuwa vile ndio tatzo, nimepoteza miaka mitatu ya maisha yangu,kwanini nisingeambiwa mapema tangu nlivoripoti kama kweli watu wenye ulemavu kama wangu hawapaswi kusoma kitu fulani

Nikaanza kusoma upya kitu kingine kwa msaada, sielewi ni nini nasomea kwa maana haikikuwa kitu nlichowaza ntakuja kusomea,naishi kama sipo kwa maana bado sijapona kutoka kwenye maumivu niliopitia,nasoma kwa wasiwasi kwamba kama kwenye elimu tu nilifanyiwa vile, japo kuwa nilikuwa nafaulu vizuri lakini ulemavu wangu ukawa fimbo ya kunirudisha nyuma, je nnachosomea sasa nkimaliza ntaweza kupata kazi kwa mfumo huu?

Kila siku kwenye mikutano,matamasha na vyombo vya habari wanaongelea haki sawa,kuwezesha walemavu na kuwainua, lakini bado jamii na nyanda mbalimbali zinaamini kwamba mlemavu hawezi kuwa mtu fulani ama fulani.

Ningewezeshwa ningepewa msaada na kuinuliwa kwa bidii zangu nlizozionesha bila kujali ulemavu wangu naamini ningeweza wazungu wanasema "DISABILITY IS NOT INABILITY" serikali inatakiwa kuangalia kwa jicho la pili sera juu ya watu wenye ulemavu na changamoto naona ipo kimaneno zaidi kuliko vitendo.

Vyuo na taasisi za elimu ya juu pia zinatakiwa ziwe na miongozo ya mapema, kama ni kweli haipaswi mtu mwenye changamoto fulani kusomea kitu fulani ni bora aambiwe mapema kuliko kumpokea,kumpa moyo alafu kuja kumuacha bila kujali miaka yake aliopotezewa,afya yake ya akili na uchumi.

KAMA VILE WANAVOSEMA WALEMAVU WAKIWEZESHWA WANAWEZA ,MABADILIKO YANAHITAJIKA ILI KAULI HIO IWE YA VITENDO ZAIDI KULIKO MANENO.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…