hatedthemost
JF-Expert Member
- Oct 20, 2021
- 469
- 324
Abunuwasi si neno geni katika masikio ya walio wengi. Wanasema ni hadithi za kufikirika .Msemo ' Ndoto za Abunuwasi' wapendwa sana kutumika na watu wanaowaza yasiyowezekana, yaani mawazo ambayo ni ngumu kupitiliza kutokea katika ulimwengu huu wa nyama.
Kwenye andiko hili ,mimi nitakueleza ndoto zangu za kufikirika,ndoto zangu za Abunuwasi ;Ndoto nilizokuwa nikiota nikiwa binti mdogo ambaye hakuiona dunia katika uhalisia wake. Dunia yake ilikuwa runinga na vitabu ambavyo baba alikuwa akileta nyumbani. Kwangu,dunia ilikuwa sehemu yeyote isiyokuwa taifa hili lenye jina maarufu;'kisiwa cha amani'
Dunia ilikuwa mbali nami,nayo kufikiwa ilihitaji Safari ndefu ya ndege! Dunia kichwani mwangu ilikuwa Ulaya na nchi zingine za mbali ambazo watu walifanya makubwa na yakafanikiwa kutangazwa, dunia yangu ilikuwa kuona mifumo inayoweza kufanya kazi katika sekta mbalimbali , maajabu ya wanasayansi kama kina Albert Einstein, Isaac Newton na Ben Carson(nani asiyefahamu watenda miujiza Hawa?), maeneo ya kuvutia, barabara na bustani nzuri na mvua ya barafu. Ndoto yangu kubwa ikawa ni kuwa mtu mzima ili niweze kuondoka hapa na kuzamia katika nchi za watu weupe.
Umri unakuja na kujifunza mengi nami sijapitwa na hili. Katika miaka hii ishirini na tatu kasoro ya kuishi, nimepata kufahamu kuwa yamkini sitaki kuondoka nyumbani kwetu, sidhani kama nitaweza kuiacha familia inayonipenda na maisha haya niliyoyazoea. Miaka hii ishirini na mbili ya kuishi imenionesha vile itakuwa ngumu kuacha yote nyuma na kuiendea dunia ile niliyoitamani enzi za utoto. Miaka ishirini na mbili ya kuishi hapa imefanya nifahamu ya kuwa;dunia yangu ni taifa hili nililozaliwa.
Taifa hili limenipa marafiki wa dhati,taifa hili limenionesha sehemu nzuri na za kuvutia ambazo zinawaleta watu kutoka mbali,nina mapenzi ya dhati na Tanzania !
Mapenzi yangu kwa taifa hili ni kama mapenzi ya mama aliemuona mtoto wa kumzaa kwa mara ya kwanza nae haishi kumtazama . Mapenzi yangu ni kama kumuona mtoto wako akianza kukaa nawe huishiwi na matumaini kuwa iko siku mtoto huyo atatambaa, atatembea na mwishowe kukimbia nawe utakua mtu mwenye furaha kuu.
.
Mtoto kutambaa, kutembea na kukimbia ni Tanzania mpya ninayoitizamia miaka kadhaa ijayo endapo nitafanikiwa kuiona. Tanzania nitakayoiishi nikielekea utu uzima,uzee na mwisho mwema kama tukipewa nafasi hiyo. Tanzania ninaitazamia waweza tena kuiita ndoto yangu mpya ya Abunuwasi!
Ninatazamia mifumo inayofanya kazi,mifumo ambayo haitufanyi tukimbie nyumbani na kuacha tuwapendao na yote tuliyohangaikia.
Miaka kadhaa ijayo natazamia kuona mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu ambayo ni mzizi wa mambo mengi mazuri. Ninatamani kuona hadhi ya elimu inaongezeka na elimu isiwe vyeti visivyo na Maana. Wasomi wa taifa hili waonekane huko duniani.Katika kufanikisha hili, ni muhimu kama ambavyo wanafunzi hupewa mitihani basi wenye dhamana ya kufundisha mashuleni mpaka vyuoni kupimwa Kila baada ya muda ili kujiridhisha na utoaji wa elimu iliyo bora.
Afya ni kama moyo taifa hili. Ninatazamania sera ya ‘bima ya afya kwa wote’ ikitimizwa huku magonjwa kama saratani na magonjwa ya figo yakijumuishwa.Uboreshaji wa mazingira ya wafanyakazi wa afya usiachwe nyuma kamwe!. Mazingira hayo ni pamoja na mishahara inayofaa na kuongezwa Kwa idadi ya waajiriwa Ili kupunguza mzigo wa kazi kwa wafanyakazi wachache walioko. Vijana wengi wako wakizunguka na ujuzi wao katika kada mbalimbali za afya bila matumaini ya kuutumia.
Katika sekta ya afya kuna magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kama vile kisukari aina ya pili na shinikizo la damu. Magonjwa haya yameonesha kuathiri watu wazima wengi. Mojawapo ya kinga ya magonjwa haya ni mazoezi ya mwili. Zoezi la kutembea ni zoezi zuri Sana kwa watu Rika Zote. Swali ni? watu hawa watapata wapi hamasa ya kutembea zaidi kama barabara zilizo hazina sehemu maalumu kwaajili ya watembea Kwa miguu? Tunawekeza kwenye tiba na sherehe za kuadhimisha magonjwa tusisahau kueka nguvu zaidi katika kwenye kinga ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwa namna kama hii.
Mazingira ni sehemu muhimu sana na taifa lilipeleka vijana wengi katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi huko Dubai. Lakini je tunayaishi tunayoyaendea katika mkutano? Kutupa taka katika sehemu zisizo maalumu ni kosa. Lakini ziko wapi pipa katika maeneo mbali mbali ya miji kuhakikisha watuu wanazo sehemu za kutupa Taka? Ninatazamania kuona miji yenye mapipa ya taka Ili kusaidia kupambana na utupaji wa taka hovyo. Ninatamani kuona ukusanyaji wa taka majumbani na sehemu za biashara ifanyike kwa wakati kama ambavyo pesa kwaajili hii huja kuchukuliwa kwa wakati. Taifa lina wataalamu tele wa afya ya mazingira ni muhimu sana kuwatumia hawa katika kuhakikisha hilo.
Ninaipenda Tanzania,Dunia yangu ni hapa!nami ninayo matumaini na taifa hili lakini ninawezaje kama kijana kujiajiri kama ambavyo tunaambiwa? Kodi hazilipiki,na mara nyingine kumekuweko na kodi nyingi kiasi kwamba tunatafuta ‘njia za panya’ japo tubaki na chochote Cha kuendesha maisha. Kijana mdogo alipe ushuru wa bandari na kodi zingine,alipie kodi ya jengo Kwa serikali na wenye mtumba,akituma pesa ni kodi na akipenda kutoa ni kodi,akilipa umeme kodi,taka nayo analipa kodi,akiweka bango katika biashara ni kodi na akitaka kutangaza mitandaoni ni kodi. Je Ni kweli lengo Ni kuona vijana wanajiajiri? Mifumo ya ukusanyaji kodi ihamasishe watu kulipa kodi kwa moyo.
Kila ninapoongea na watu napata kusikia kuwa ndoto zangu juu ya taifa hili ni za kufikirika lakini mimi nina ndoto! Katika andiko hili nimeandika machache ninayoyatamani na ni imani yangu kuwa ndoto hii itatimia nikiwa hai,nami nizidi kulipenda taifa langu la kujivunia Utanzania wangu.
Tanzania ya kufikirika!! Tanzania itakayofanya tusitamani nchi za mbali, kwani inawezekana kuwa na mifumo inayofanya kazi hapa.Dunia ni hapa ! Dunia yangu ni Tanzania na si ndoto za Abunuwasi.
NB😛icha ni katika nyingi ninazopenda kupiga.

Upvote
1