jamesmwakalinga
Member
- Oct 17, 2024
- 6
- 7
Ndoto za kada maarufu wa chama cha mapinduzi CCM)jimbo la moshi mjini za kuchukua fomu kuomba ridhaa ya chama chake kimteue kuwania ubunge kupitia jimbo la moshi mjini ,zimeyeyuka kutokana na kuwa chini ya adhabu.
Mapema mwaka huu,kada huyo alipewa onyo na chama chake kutokana na kuendesha siasa chafu zinazoenda kinyume na kanuni na maadili za ccm na jumuiya zake toleo la mwaka 2022.
kilichomponza kada huyo ni kutengeneza kundi la WhatsApp ambalo lilikuwa mahususi kwa ajili ya kukashifu viongzi wa chama wilaya na mkoa akiwamo mbunge wa sasa,Priscus Tarimo anayetokana na ccm.
Mbali na hilo,kada huyo anadaiwa kutoa misaada kwa vikundi vya kina mama wajane,misibani na kwingineko ,zawadi na vitu mbali mbali ambavyo ni kinyume na kanuni ya 6(2)(C)ambayo imetoa katazo kwa mwanachama wa ccm ambaye anania ya kugombea nafasi ya uongozi kwenye eneo husika.
Kanuni hiyo katika kipengele C imeainisha mambo ambayo mwanachama haruhusiwi kuyafanya na hapa inasomeka hivi,
"kutoa michango,misaada na zawadi za vifaa au nyenzo kwa mtu au shughuli yeyote mpaka iwe tu kwa ridhaa ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya ngazi inayohusika kwa masharti kwamba kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa inapata taarifa",inasema kanuni hiyo na kuongeza..
"Kutoa michango,misaada,zawadi nk katika eneo ambako mwanachama huyo anakusudia kugombea nafasi yeyote ya uongozi na endapo katika mazingira maalumu ruhusa imetolewa mchango huo hupokelewa kama ilivyofafanuliwa katika vifungu 6 (2)(a) na 6(2)(b) basi mchango huo hautatangazwa.