Ndoto za kweli

malisak

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2006
Posts
694
Reaction score
775
Binafsi sikuwahi kufikiria kabisa kuhusu ndoto. Nilikuwa nachukulia kama mauza uzaza ya uchovu na mawazo ya siku nzima. Ila kuna kitu nimekuja kukigundua kwa namna mbili kwanza ni kuwa sina kawaida ya kuota ota kila wakati na ikitokea naota basi hiyo ndoto inakuwa kweli. Mfano nikiota mtu fulani anaumwa basi ataumwa kweli, fulani kafa basi atakufa kweli na pia na weza kumwona mtu kwenye ndoto na kesho yake nikamwona kweli hii n i kitu ya kawaida?, kuna mtumishi mmoja wa Kiroho niliwahi kumuuliza akaniambia nisimulie mtu lakini najaribu kuwaza hii hofu inayonipata nashindwa inabidi kuuliza nipate amani. Niliwahi kumwota dereva wa kazini anaumwa nikamsimulia asubuhi yake mchana kaanza kuumwa sana mpk akalazwa alinichukia mpk kuitwa mchanawi. Hili swala ni la kizahania, saikolojia, mapepo au nini maana imani yangu ilikuwa dhaifu sana kukubaliana na haya mambo ila now naona naishi kwa mashaka hata nikisali sana kabla ya kulala kama kuna issue zinakuja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…