Deadbody
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 4,274
- 6,595
Hakika akili ile huwa ni ya kiwango cha phD ambapo mbetiji hakosei kabisa kupanga mpangilio wa mambo atakayofanya kama mkeka wake ukitiki:
Mimi nikibet huwa natengeneza mkeka unaanzia million 35 kwa 500 tu na kabla hata timu haijaanza kucheza huwa nawaza mambo mengi nitakayoyafanya kupitia hela hiyo kama nikiipata
Mfano wa mambo ambayo huwa nayawaza ni :
- Kununua nyumba
- kununua gari
- Kuoa msichana mzuri kushinda wote huku UKONGA
- Kujiendeleza Kielimu
- Kuwasaidia ndugu,jamaa na marafiki
- Kuwa mtu wa starehe
- Kumtolea mungu sadaka
- Kuwa mtu wa Pamba za kisasa zaidi
Hakika tunaobeti tuna akili sana ya maisha ila tu wachawi wengi wamejificha kwenye mkeka
Wewe mwanaJF ambaye huwezi pitisha siku bila kubet huwa unawaza mambo gani utayatimiza kama mkeka wako ukitiki?