IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
Katika mchezo wa mpira wa Miguu timu pinzani inapopungukiwa wachezaji uwanjani huleta ahueni kwa mashabiki wa timu ya waliyo wengi. Ipo kasumba kwamba kupungua idadi ya wachezaji uwanjani huidhoofisha timu iliyooungukiwa na kufanya iwe rahisi kuifunga.Hali hii hujenga natarajio chanya kwa mashibi wa timu ya waliowengi hasa kama walikuwa nyuma kwa mabao. Hata hivyo, historia inaonyesha kuwa hata wachezaji wakiwa wachache bado wana uwezo wa kuwafunga walio wengi. Japo sikumbuki ni mechi ipi lakini walibaki wachezaji saba tu uwanjani na wakaweza kuwafunga wenzao waliokuwa wamesalia kumi. Wanasaikolojia watasema kupungua kwa idadi ya wachezaji hufanya timu iliyoppungukiwa kupata ari na mhemko wa utambuzi kuwa wapo wachache na kila mmoja kujibidiisha kucheza kwa ajili yake na kwa ajili ya pengo la asiyekuwepo.
Kimsingi, uwingi wa watu-iwe wachezaji au wananchi haijawahi kuwa njia pekee ya kupata ushindi au kufanikiwa kitu. Mfano mzuri ni sera za vijiji vya ujamaa na mashamba ya kijamaa ambazo hazikutosogeza popote kiuchumi pamoja na uwingi wa walimaji. Historia inaonyesha kuwa ni watu wachache ndiyo mara nyingi hupata nguvu ya kuwa juu ya wale wengi (the minority became the majority). Mfano wakoloni (wachache) waliweza kuwadhibiti waafrika (wengi), Polisi (wachache) wanaweza kuwadhibiti wanachi (wengi)...Ni wagunduzi (wachache) wanaweza kunufaisha watu (wengi). Kumbe hoja hapa si uwingi bali nyenzo na fikra thabiti.
Nchini Marekani, kuna hofu kuwa baada ya miaka michache ijayo idadi ya watoto wa kizungu itakuwa pungufu ya watoto wa rangi nyingine. Wengine hutoa hii kama sababu ya hofu ya wazungu kuendeleza ubaguzi hasa kwa weusi ( ambao kama tujuavyo wanajua kutumia vizuri viuno vyao), kwamba ongezeko lao kwa kasi ni hatari kwa utambulisho 'identiy' yao. Hoja hizi sinashabikiwa na weusi wengi ambao tena wengine ni wasomi sanasana. Lakini watu hao hao wanasahau kuwa ni wazungu haohao kwa uchache wao walikuja wakawatumikisha na kisha wakawasomba mababu zao kuwapeleka Ulaya kuwatumikisha zaidi. Meli moja kwa mfano iliweza kubeba watumwa 200 huku wazungu wakiwa chini ya 10. Hoja hapa si uwingi bali nyezo (mashua, bunduki na minyororo) na akili ya kutambua jinsi ya kuwatumikisha weusi.
Kwa muktadha huu, binafsi sioni tishio la weusi kwa wazungu hata wakiwa kumi elfu kwa 100. Wenzetu wanatuzidi kwa kuwekeza katika Nyenzo na akili wakati weusi wanang'ang'ana kujiwezesha kwa kuongeza idadi yao... Pasipo kuwezesha watoto wao kuwa wagunduzi (wa nyenzo) na akili ya kutambua mwelekeo wa dunia na fursa za kisayansi, itakuwa ndoto kuondoa dola-tawala ya kizungu dhidi ya rangi nyingine.
Yangu ni hayo tu kwa leo
.