Ndoto zangu za kuwa tajiri naona zinakwenda kutimia

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Baada ya miaka 6 mbele nitamiliki restaurent 6 za milioni 40 katika nchi mbali mbali hapa East Africa
Uganda, Tanzania, Kenya, DRC, Burundi, na Rwanda

Na RESTAURENT zangu zote zitaitwa jina moja la ANABEL na logo yake ni alama ya vidole 2 juu tukutane mwezi wa 4 2023 Dar es Salaam

Siri ya mafanikio ni kutafuta pesa kwa bidii

Na kuweka Record nzuri benki ili siku ukiwa na wazo lako la biashara benki waweze kukukopesha pesa ili utimize ndoto yako

Wewe endelea kupenda wanawake mwisho utaishia kutuita mafreemason bure na wakati wenzako hatulali kisa Kutafuta pesa
 
Kumbe bado una ndoto.

Ndoto zitabaki kuwa ndoto mpaka siku ITOKEE kweli
 
Baada ya miaka 6 mbele nitamiliki restaurent 6 za milioni 40 katika nchi mbali mbali hapa East Africa
Uganda, Tanzania, Kenya, drc, burundi, na Rwanda...

Wazee mnaandaliwa kutapeliwa
 
Aliyekwambia wanawake wanamaliza hela nani? Uliza matajiri walivyo na warembo na wanawanunulia vitu hawahongi 30,000 na 50,000.
 
Utajiri wa ndotoni unaudhi sana pale unaposhtuka usingizini ukijikuta upo geto na madeni mpaka miguuni
 
Baada ya miaka 6 mbele nitamiliki restaurent 6 za milioni 40 katika nchi mbali mbali hapa East Africa
Uganda, Tanzania, Kenya, drc, burundi, na Rwanda...
Ulipokosea ni hapo kupangia watu cha kufanya! Una uhakika kila mtu anataka kuwa tajiri? 😃😃😃 Wewe piga kazi ukijenga sawa, mwenzio akilewa sawa lakini maswala ya kufanikiwa ukaanza kutupiga madongo eti tunapenda wanawake huo ni unafiki!

The Goal of life is Happiness
Shughulika na yako, maisha ni yako!
Kila la kheri mkuu , Mungu akuongoze ufanikiwe
 
Amefanikiwa wapi huyo alikuwa anaota tu nimemwambia amka kitandani katafute mlo wa siku ni lini umesikia aliyefanikiwa anajitangaza
 
We kufanikiwa sahau
 
Iwe kheri natambua wapambanaji ndoto zetu n kubwa mno hope mipango yako iende sawa uweze kuajiri vijana wengine keep it up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…