Ndoto zinavyoyasumbua maisha yangu, Nifanye nini?

Ndoto zinavyoyasumbua maisha yangu, Nifanye nini?

Giltami

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,038
Reaction score
1,623
Nikipata muda naweza andika historia ya maisha yangu kwa kirefu, Kwa sasa naomba nieleze kwa ufupi. Nilipokuwa kama darasa la tatu au la nne hivi nilikuwa nalala na kaka nyumba ya pembeni kama mnavyojua nyumba za vijijini basi tulilima alizeti tukavuna kidogo tukawa tumeiweka pembeni ya nyumba kukawa umbali wa kama mita 20 tunachambua maharage, tulikuwa mimi na dada zangu wawili na mtoto wa mjomba jumla watano na mtoto wa jirani.

Siku hiyo ilikuwa Jumamosi sasa Ijumaa kuamkia hiyo Jumamosi nikiwa nimelala niliota ndoto nimemuona nyoka mkubwa akiwa mlangoni mwetu tunapolala na kaka basi niliposhtuka nikajua ni ndoto tu nitapotea. Sasa hiyo Jumamosi tunaendelea na kazi na kutaniana hapa na pale kama kuna sauti ikanambia geuka mlangoni kwenu aseee sikuamini nilimuona nyoka mkubwa sana kifuto wa njano yule wa ndotoni akitoka kwenye zile alizeti anaingia ndani kwetu nikawaambia nyoka wote wakashtuka nikawauliza wakasema hawajamuona cha ajabu hakuna aliyemuona mimi niliyekuwa nimempa mgongo iwaje nimuone nikashangaa sote tukajua anatafuta mayai huyo bro hakuwepo tuliita watu lakini waliogopa kuingia kumuua niliingia nikapanda kitandani na wengine wakaja tukamuua, kilichofuata kwa week kama 2 nyoka wadogo walifululiza eneo la geto letu na niliwaua bila kuogopa.

Hayo na mengine mengi ni enzi za shule ya msingi, sasa baada ya kukua nikiwa umri wa ujana ndoto zikarudi tena niliota kama msiba baada ya kama mwezi mzazi wangu alifariki, kilichofuata ni kama kuna kitu kina control maisha. Niliota tena msiba ukatokea, nawaona sana nyoka ndotoni ,kosa niote ndoto na niikumbuke inaniumiza maana najua ni suala la muda tu itatokea nilichoota week mbili zimepita niliota nagombana na mdada jirani napoishi niliumia maana yule dada alikuwa ananiheshimu sana hivi navyoandika hapa yule dada niliyemuota kaniundia uongo mbaya sielewani nae

Kwangu ndoto inanipa taarifa ya siku zijazo nini kitatokea ila why matukio mabaya ndio naota sana, nikaamua kunywa sana pombe kabla ya kulala kweli nikifanya hivi sioti ila itatokea siku nitajisahau na kunywa kidogo nikilala tu naota ndoto tena. kwangu zinaniumiza sana.
 
Utaendelea kuteseka Hadi siku utakayotambua kuwa kinywa chako kina ukuu mkubwa wa kugeuza mabaya kuwa mazuri, Kaa chini kwa Dini yako omba kulingana na ndoto uliyoota na kutamka. Mazuri.
Ukiwa mnyonge utaendelea kuwa hivyohivyo maisha yako yote, kujiamini huanzia ndani kwenda nje
 
Nipo kama wewe ila mimi hua natengua kwa maombi na hicho kitu hakitokei ila before zilikua zinatokea sana now dayz naacha nzuri tu

Sasa wewe umesema ni mlevi sijui tunafanyeje apo
 
Nipo kama wewe ila mimi hua natengua kwa maombi na hicho kitu hakitokei ila before zilikua zinatokea sana now dayz naacha nzuri tu

Sasa wewe umesema ni mlevi sijui tunafanyeje apo
😅😅Sio ulevi mkuu ni unywaji napotaka nisiote na nilale mpaka asubuhi kwa amani
 
Back
Top Bottom