NDOTO

boblyy sams

Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
26
Reaction score
32
Habari zenu,,
Ilikuwa majira ya saa nane mchana, nilikuwa nipo kwenye treni ya umeme nikitokea mbagala ambayo ilikuwa mithili ya jiji la washington d.c nikielekea zangu k. koo ambayo ilkuwa imegubikwa na maghorofa marefu kama vile dubai,,nililazimika kutumia public transport yaani treni ya umeme kwani gari langu aina ya ferrari alienda nalo mdogo wangu shuleni(B.Mkapa Sec School), nilifanya mizunguko yangu ya hapa na pale na muda wa kurudi nyumbani uliwadia.Kwa kuwa muda huo ulikuwa ni muda wa mdogo wangu kutoka shule,, nilichukua tablet aina ya sams ambazo zilikuwa zinatengenezwa hapa hapa tanzania maeneo ya vingunguti, nilimtafuta mdogo wangu akaniambia yupo workshop wanatengeneza robot wa kucontrol magari barabarani, kwakuwa nilionyesha kutomuamini kwani muda wa kurudi nyumbani ulikuwa tayari basi alipiga selfie na teacher akanitumia, nilivyoipakua nilijiridhisha kweli yupo workshop internet ilikuwa na kasi ya 10G na public wifi ilikuwa available kila sehemu,ila nikaona bora nimpitie tu dogo nilipofika benja nilipanda lift mpaka floor ya 30 ndo lilipo darasa la dogo,nikawakuta wanapata chakula cha jioni, ulikuwa ni msosi wa hatari, meza ilichafuka mithili wapo serena hotel ila kama ilivyoada wanafunzi hawapendi chakula cha shule, basi dogo aliacha menu nikaongozana nae kurudi mbagala, tuliamua kupitia njia ya underground iliyotoka shule ya uhuru via keko mpaka kizuiani,jiji lilikuwa limejengeka sana kwani zakhiem ilikuwa mithili ya las vegas, ile nafika rangi 3 nilishitushwa na horn za magari na ndipo niliamka usingizini,,, Oooppss kumbe nimefika mbagala after kusota kwenye foleni kwa masaa takribani 7 nikitokea k.koo
NDOTO HIZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…