Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
MHE NDUGA, SPIKA MSTAAFU ALIVUNJA MILA NA DESTURI ZA CCM NDIYO MAANA WENGINE IMEWACHUKUA MDA KUELEWA.
Na Elius Ndabila.
0768239284
Kwanza nianze kwa kumpongeza Mhe Ndugai kwa kujiuzulu nafasi ya Uspika. Ametimiza moja ya nguzo mhimu kiongozi bora kuwa anapokosea anapaswa kuwajibika. Accountabilities and Responsibilities ni nguzo mhimu katika utawala bora. Hongera Mhe Ndugai!
Wakati wa sakata hili kuliibuka makundi kadhaa wa kadhaa. Kundi la kwanza lilimshauri Mhe Ndugai ajiuzulu, kundi la pili lilisema asijiuzulu hana kosa, kundi la tatu lilisema tuzungumze maendeleo na tujibu hoja za Mhe Ndugai. Hawa walikuwa wakimtetea Kwa kutumia katiba ya nchi. Yaani walitaka tutatue changamoto za CCM Kwa kutumia Katiba ya nchi.
Leo nitazungumza kwa ufupi na kundi lililomtetea na la mwisho lililosema tuzungumze maendeleo tuachane na Mhe Ndugai.
Mila na Desturi za CCM ndizo zinazojenga umadhubuti wa CCM na misingi imara ya CCM. Mhe Ndugai alikiuka mila na desturi za CCM ndiyo maana hata kujiuzulu barua ametuma kwa Katibu wa CCM na nakala akapeleka Kwa Katibu wa Bunge. Angevunja katiba ya Nchi barua angempelekea Katibu wa Bunge na nakala angempelekea Katibu wa CCM. Sijui kama mnanielewa.
Mila na Desturi ya CCM ni kuwa huruhusiwi kumpinga kiongozi hadharani Kwa jambo ambalo wewe ungeweza kukaa na kumshauri.
Mhe Ndugai alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu, ambayo Mwenyekiti wake ni Rais Mhe Samia Suluhu Hassani. Kamati Kuu ndiyo kikao Cha Mwisho Cha CCM. Ndicho kikao chenye mipango yote ya nchi. Ndicho kikao kinachomshauri Mwenyekiti ambaye ni Rais ninaweza kusema kwenye kila Jambo. Kwa msingi huo kamati kuu ndiyo injini ya Rais. Hivyo kwa mila na desturi kauli aliyoisema Mhe Ndugai hata kama ilikuwa na faida kwa nchi hakupaswa kuisema Kwa kuwa ilikuwa inakinzana na kauli ya Mwenyekiti ambaye ni Rais wa nchi.
Kwa mfano Baraza la Mawaziri wakishafanya baraza uwe umekubaliana na mazimio au hujakubaliana maadamu baraza limeisha unapaswa kwenda kuyasema yaliyoazimiwa si Yale ambayo wewe ulikuwa unatetea. Kufanya hivyo unapaswa ujiuzulu, rejea sakata la Chavda lilivyomuondoa mzee Mrema.
Kwa mkutadha huo, Mhe Ndugai alikiuka Imani ya CCM ambayo inajengwe kwenye misingi ya Mila na desturi. CCM imeendelea kudumu madarakani Kwa kulinda Mila na desturi ambazo ndizo tunu za Chama Chetu.
Ninaamini Kwa watetezi andiko hili fupi litajaribu kuwafungua macho.
Kazi Iendelee!