Kila mmoja mwenye akili timamu amepatwa na mshangao jinsi kiongozi huyu wa muhimili muhimu wa bunge kubadilika ghafla. Tanzania tuna bahati mbaya kupata kiongozi mnafiki kwenye uongozi wa juu kama bunge. Huyu mtanzania mwenzetu ana kibuli sana kama alivyokuwa Godfather wake. Nikikumbuka alivyomdhalilisha professor Assad machozi huwa yananitoka. Mambo anayoongea leo ndugai kama changamoto kwa taifa yamepita bungeni ambapo yeye ndio kiongozi wa mijadala. Ndugai ameharibu bunge letu kuruhusu mijadala ya majungu leo anaongea. Kubadilika kwa ndugai kuna walakini either hana maelewano mazuri na Rais wa sasa au anatafuta umaarufu wa kisiasa ili uwe mtaji wake kwenye kugombea presidential post 2025
133.-(1) Spika atakoma kushika nafasi ya madaraka ya Spika
litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a) atachaguliwa kuwa Mbunge;
(b)
kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika,
lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze
sifa za uchaguzi wa Spika;
(c)
ataondolewa kwenye madaraka ya Spika kwa Azimio la
Bunge lililoungwa mkono na Wabunge ambao idadi yao
haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote;
(d) atashindwa kuwasilisha tamko rasmi kuhusiana na mali na
madeni yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(e) atapatikana na hatia kwa kosa la kutoa habari za uongo, kwa
kiapo kinyume cha sheria kuhusu tamko rasmi lolote
lililotolewa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
(f) atashindwa kuwasilisha taarifa ya mali kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii kabla ya kumalizika muda uliowekwa
kwa ajili hiyo;
(g) itathibitika kuwa amevunja masharti ya sheria inayohusu
maadili ya uongozi wa umma; au
(h) kufariki dunia.
(2) Isipokuwa shughuli ya kumchagua Spika, hakuna shughuli
yoyote itakayotekelezwa katika Bunge wakati wowote ambao nafasi ya
madaraka ya Spika itakuwa wazi.