Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

Ndugai: Lishe duni ya wachezaji wetu imechangia Taifa Stars kufungwa

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,588
Reaction score
11,668
Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia Stars kupoteza mchezo wa kwanza jana dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu.

Spika Ndugai ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Misri aliposhuhudia mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Tanzania uliomalizika kwa Taifa Stars kuchapwa 2-0.

Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.

"Kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji wetu lishe nzuri ya kutosha ili kushindana na wapinzani wa aina ya Senegal," alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.

Source : Mwananchi

====

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema hakwenda Misri yeye kama yeye, bali alitumwa na Rais John Magufuli kwenda kuiwakilisha nchi.
Spika Ndugai ameyasema hayo leo Jumanne Juni 25, 2019 alipokuwa akifafanua kauli ya aliyemuita kiongozi mmoja mmoja wa Serikali kuwatuhumu baadhi ya wabunge kuwa wamewalaumu wachezaji na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Amesema: “Mimi nimetumwa Misri na Rais, halafu anakuja mkuu wa mkoa mmoja ananisumbua, siwezi kusumbuliwa na mkuu wa mkoa mmoja.”
Amesema kiongozi huyo wa Serikali amezungumza maneno yasiyofaa kuhusu Bunge la Tanzania na wabunge na kumdanganya hadharani Rais Magufuli, kuwa wawakilishi hao wa wananchi wamewadhihaki wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Spika huyo amesema hawezi kusumbuliwa na mkuu wa mkoa mmoja, kwa kuwa anatambua nini anakifanya.
Pia Soma
Amesema kati ya wabunge waliokwenda Misri ambako timu ya Taifa inashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), hakuna aliyemlaumu mchezaji yeyote wala kuisema vibaya timu hiyo.
“Hayo ni mawazo ya mtu ambaye kidogo ndiyo hivyo. Ni bahati mbaya sana tuna viongozi wa Serikali wanadiriki kumdanganya Rais hadharani, kiongozi wa Serikali unapoongea mbele ya rais jipange uongea ukweli mtupu wa mwenyezi Mungu, usisingizie wala kumuonea mtu hatufanyi hivyo.”
Mapema leo asubuhi, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika ufunguzi wa Mradi wa Gesi, Kigamboni jijini humo, alisema ameshangaa wadau mbalimbali ambao wameizungumzia vibaya timu hiyo baada ya kupoteza mbele ya Senegal.
“Nimeumizwa na matokeo ya Taifa Stars, lakini nimeumizwa zaidi kwa watu kuwabeza wachezaji wetu ambao wametubeba Watanzania ambao ndani ya miaka 30, haikuwezekana lakini wao wamepambana mpaka tupo Afcon leo hii," alisema Makonda
Makonda alisema alizungumza na wachezaji hao pamoja na nahodha Mbwana Samatta na wamemuhakikishia kwamba watafanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Kenya.
"Sisi Afrika Mashariki tunajuana vizuri kwahiyo Mhesimiwa Rais wala usiwe na wasiwasi tutafanya vizuri katika mchezo huu ambao tunahitaji ushindi na wachezaji wapo vizuri," alisema Makonda.
Aliongeza iwapo Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aweze kutoa neno lolote la kuwapa moyo kuelekea katika mchezo ujao.
Tanzania itacheza na Kenya Alhamisi mchezo utakaopigwa saa kumi na moja jioni.
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia Stars kupoteza mchezo wa kwanza jana dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu.

Spika Ndugai ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Misri aliposhuhudia mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal na Tanzania uliomalizika kwa Taifa Stars kuchapwa 2-0.

Ndugai alisema ukiangalia kwa umakini utaona wale wachezaji wa timu pinzani walikuwa na miili mizuri ambayo inatokana na lishe nzuri.

"Kuna umuhimu wa kuwapa wachezaji wetu lishe nzuri ya kutosha ili kushindana na wapinzani wa aina ya Senegal," alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza.
 
Mambo ya udumavu unaosababishwa na lishe duni upo lakini pia ni species za kitanzania,waganda wana Vimo vya average ya John Boko lakini waliwamudu wakongo wenye miili dizaini ya Senegal urefu na unene
Ko sio sahihi moja kwa moja kusema hiyo ndio sababu,kwa mpira gani tuliocheza hadi hiyo iwe sababu? Species za West/Central and North Africa ni giants kuliko east Africa anbapo wengi ni moderate,wasukuma ni jamii ya west africa
 
Dah inasikitisha sana. Yaani tunashindana kuiponda timu yetu wenyewe? Kama Spika kasema haya kakosea sana.

Timu yetu ilijitahidi na hicho ndicho walichopata. Tuwatie moyo kwa michezo ijayo na tujifunze kwa wenzetu namna wanavyoweza
 
Amegundua Hili baada ya kufungwa?
Na siyo huyu tu. Watatokea ''wataalam'' wengi sana ku-analyse sababu ya kufungwa. Tu nchi ya watu watu wa ajabu sijawahi kuona. Tumefanana na yale manyani kwenye hadithi yanakumbuka kuambiana kujenga nyumba kila inyashapo mvua lakini mara ikiacha yanasahau. Tanzania haitaweza kuendelea kimpira kwa kutumia ujanja ujanja na short cut. Mpira hujifunzwa tangu utotoni. Kwa nini tunashindwa kuanzisha Football Academy School hata tatu tu kwa kuanzia moja iwe eg Mwanza, nyingine Dar na ya mwisho Mbeya. Hizi shule zichukue watoto wa miaka 7 waanze darasa la kwanza huku soccer ikiwa kama major yao. Wasome na masomo mengine ya kawaida. Tuwaendeleze mpaka watakapofikia miaka 18, 19 hadi ishirini hatutakosa wachezaji wazuri kama thelathini hadi arobaini hivi. Bila kufanya hivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu tu! Wenzetu ndivyo wanavyofanya! Ni miaka kama kumi tu tutaanza kuona matokeo yake!
 
Back
Top Bottom