Ndugai: Ndoto ya Mihimili huru rasmi Imeyeyuka

Ndugai: Ndoto ya Mihimili huru rasmi Imeyeyuka

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kama taifa yaweza kuwa tuko katika hali mbaya zaidi kufuatia kuachia ngazi kwa spika Ndugai.

Ni wazi kuwa Ndugai yamemkuta.

Ndugai kapigwa na kitu kizito utosini!

Hakuna asiyejua Ndugai alikuwa mtu wa hovyo.

Hata hivyo mtu huyu kafurushwa kwa sababu ya kutoa maoni yake. Agenda hii ni yetu ya msingi ambayo hatutakoma kuidai.

Kwa yaliyomkuta Ndugai nani yuko salama?

Ndugai hakutendewa haki. Kwa kutokutendewa haki fursa na ndoto za kupata:

1. Utawala na mihimili yenye uhuru kamili
2. Watawala kuwapo madarakani kwa ridhaa ya wananchi
3. Watawala kuwajibika kwa wananchi
4. Kuzaliwa kwa katiba mpya ya wananchi.
5. Kuzaliwa kwa Tanzania mpya.

kwa sasa zimeyeyuka. Tumerudishwa nyuma zaidi sana ya tulipokuwa jana.

Hatuna cha kushangilia kwenye hali hii.

Ndugai amekwenda, agenda yetu iko pale pale.

Aluta Continua!
________

Angalizo: "kushabikia kwenye kadhia hii, yaweza kuwa ni heri ya nyani kushangilia miti kuungua."
 
Haya mapambano siku zote huwa ni jumuishi, yanahitaji uwepo wa watu au makundi mbalimbali ili kufikia malengo.

Unaposema ndoto ya mihimili huru imeyeyuka umekata tamaa mapema sana, hii ndoto haikuanzishwa na Ndugai na haitafia kwa Ndugai.

Mihimili huru itapatikana kwa Katiba Mpya na kwa maoni yangu mambo yanaenda vizuri, lililotokea kurithisha urais kuona haki zinavyokandamizwa, mfano tumeona Chalamila kashtuka hii kwangu ni alama nzuri.

Badala ya kusema mambo yanakuwa magumu, ndio tunatakiwa kusonga mbele zaidi, hakuna kurudi nyuma tutakuwa tunachekesha kisa Ndugai kajiuzulu.
 
Mkuu, kichwa cha mada ni habari kwa ufupi.

"Kama mtori vile nyama ziko chini."

Nikionacho hapa tulikuwa pazuri sana ila ukweli mchungu, tumepigwa.

Hitimisho kwenye mada linahusika:

Aluta Continua!
 
Back
Top Bottom