Uchaguzi 2020 Ndugu Balile na wenzako, Vyombo vyenu havipigi kura msiwachagulie wagombea na wachaguaji nini cha kuambiwa, hatutaki

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
NIMESIKILIZA tamko la jukwaa la wahariri Tanzania kupitia ndugu Balile wakidai kuwa hawataripoti matusi ya wagombea, sisi wanachi tungependa kuwajulisha nyinyi wahariri ya kuwa msituchagulie nini cha kusikiliza na msiwachagulie wagombea nini cha kutueleza sisi.

Kama matusi ni sehemu ya sera basi acha sisi tuambiwe nyinyi kazi yenu ni kuripoti na si vinginevyo.

Mbona mnaripoti habari za mwanamke mmoja kubakwa na midume minne kwa kutumia kondom?

Sisi wananchi tunazo akili msituchagulie mtuache sisi tuchague mbichi na mbivu.

Mnapokimbilia tunapojua wagombea wakisema uongozi uliopita haukufaa nyie mtasema hayo ni matusi kisa utawala HUO ulilipa sanaa madeni ya jamhuri.
 
Matusi hayakubaliki mkuu
Naona kuna jitihada za kuleta maana mpya ya neno matusi.
Tangu Mgombea Urais Tundu Lissu arejee nchini na kuzunguka kutafuta wadhamini, sijamsikia akiongea maneno ambayo siwezi kuyasikiliza nikiwa pamoja na watoto wangu.
Maana, kamwe siwezi kuvumilia matusi.
Lakini nimewahi kumsikia Mgombea Urais John Magufuli, hadharani, akimwambia Mhandisi wa Maji Masasi kuwa, "wewe ni mpumbavu sana''!!!
Sikumsikia Balile akitoa tamko la kukemea matusi.
Kwa bahati nzuri, watu walio na uhuru kamili, wametumia Sayansi na Teknolijia kuhakisha kuwa taarifa na habari zote zinapatikana kiganjani.
Magazeti hayana wasomaji siku hizi.
Nina hakika Balile anajua kwamba "magazeti ni habari za mwaka 47"!!
Pole sana Balile.
 
Ni kweli kama ilivo kwa uhuru na taifa letu, wahache kutushawishi kumchagua fulani, magazeti ayo yajue hayatapiga kura katu.
 
Katika mtanange huu tunategemea watu watanadi sera zao, watu wataonyesha ubovu wa wapinza ni wao. Sasa unaposema mtu asimu-attack mtu hapo ndio penye utata. Ubovu uko kwenye sera na pia utendaji pamoja na kukiuka katiba na sheria. Kwa mfano mtu anaekuja na sheria zake na kutaka lazima wengine wazifuate na ni kinyume cha sheria na katiba yetu akiitwa dikiteta utasema katukanwa?

Kuna tatizo la mazoea, watanzania huko nyuma kuna lugha tumezizoea sasa mtu akija na lugha tofauti utasikia ametukana wakati kwa mtu mwingine haoni tusi. Hatukuzoea kwa ujumla kumsikia raisi ana nangwa, sasa raisi wetu akinangwa watu wanapiga kelele, kuwa katukanwa.

Uvumilivu unatakiwa pande zote lakini si sawa kwa wahariri kutishia vyama vya siasa na kutaka kuvielekeza nini kisemwe. Wahariri hawa hawa ambao wamemute, mambo yanatokea mbele yao wao hawa yaoni. Hakuna jipya kama hawataki wafunge kabisa au wahamie huko wanako ona kuko shwari.
 
Balile namkumbusha tu kwamba mhaya mwenzake mzee Rugemarila yuko lupango bila kosa.
Acha kuleta ukabila.. huwa wepesi sana kujisahau chadomo.. wengine wakifanya ukabila mtaanza mdomo.
 
Kwa desturi zetu na tafsiri zetu kuhusu matusi, nadhani kwa wagombea wetu, hakuna mgombea anayemzidi Rais Magufuli kwa matusi.

1) Alimtukana mkurugenzi wa halmashauri kwenye mkutano wa hadhara kuwa ni mpumbavu

2) Alikiri hadharani kuwa amekuwa akimtukana Kabudi na Mpango kuwa ni wapumbavu, mara nyingi

3) Alimwambia mzee aliyempa jogoo kuwa mama yake angekuwa hajambo, angempa yule mzee wa jogoo, mama yake mzazi. Kwa desturi zetu mtoto hawezi kumtafutia mume mama yake mzazi

Na mara nyingi amewahi kutoa kauli tata za ubaguzi au amri zinazokiuka katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hadi leo hii kuna mtu anategemea mainstream media kupata habari?

Hiyo ilikua zamani, ujio wa social media ndio kifo cha mainstream media.

Leo hii kwa kutumia social media wanasiasa wanaweza ku-fight back any negative news dhidi yao na watu wakapata habari haraka iwezekanavyo.

Nina mwaka wa 6 sijawahi kusoma gazeti wala hata kulinunua.
 
Nimemsikiliza Balile nimemdharau sana. Anasema hawataandika mtu anayeongea matusi, ila mwenye tafsiri ya matusi ni Magufuli! Sijui hata anamtishia nani maana hata gazeti lake la jamuhuri halina wasomaji wa hivyo. Mpaka sasa tume ya uchaguzi ina idadi ya wapiga kura fake hilo wala hajauliza, uchaguzi wa SM wote ulinajisiwa lakini vyombo vya habari viliandika ccm ilishinda kwa kishindo. Sasa sijui anamtisha nani wakati tunajua fika vyombo vya habari haviko huru.
 
Balile angetutajia kwa mfano tusi hata moja ambalo limetoka kwa mgombea yeyote toka mchakato wa teuzi zianze.

Siyo kila mtu anatoka alikotoka eti tunataka sera hatutaki matusi, wakiulizwa alietukana kimya, tusi lenyewe holaa.

Mbona uchaguzi wa awamu hii una masharti adi maneno ya kuongea wanapangiwa wagombea? Hizo sera zinasimamiwa na kutekelezwa na watu sasa kama huwezi kumkosoa mwenye sera mbovu au aliyeshindwa kuzitekeleza kosa lipo wapi? 2015 baada ya uchaguzi tuliambiwa hakuna siasa mpaka 2020, imefika 2020 tena tunaambiwa hakuna kumtaja wala kumkosoa mtu ni kutoa sera tu jinsi utakavyofanya ukipata ridhaa. Kwanini ni amamu hii tu ndiyo tupangiane adi vya kusema kwa wananchi?
 
Huyu balire atakuwa amehongwa sio bure
Katiba ya nchi inatamka wazi kuwa kila mtu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake.Kumtukana mtu Ni kuvunja katiba. Matusi hayaruhusiwi na katiba.Hayo hakuagiza Balile Ni katiba ya nchi imeagiza

Yuko sahihi Balile. Vyombo vya habari haviwezi kuvunja katiba kwa kuandika matusi watafungiwa na TCRA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…