Snowden E
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 1,668
- 2,908
Baada ya suala la uchaguzi wa uraisi na wabunge kupamba moto. Nilianza kufanya utafiti kidogo kwa makundi tajwa kama wametimiza vigezo na masharti ya kushiriki kwenye zoezi la kuchagua viongozi.
Nili tumia njia ya maswali, na nilifanikiwa kuuliza kwa watu 100.
Swali lilikuwa moja tu.
Niliuliza...
1. Utapiga kura kuchagua kiongozi unayemtaka?
Nilihitaji jibu la NDIYO AU HAPANA.
Pia nilihitaji kujua kama jibu HAPANA, je.. kwanini iwe HAPANA?.
Ila, kabla ya kuanza utafiti, nilitarajia kuwa wengi wa ndugu, jamaa na marafiki zangu, hawana ID za mpiga kura.
Baada ya kuanza kuuliza swali, majibu yalikuwa hivi...
80% Walisema HAPANA (hawata piga kura).
15% Walisema NDIYO (watapiga kura).
5% Walikataa kujibu.
SABABU ZA WALIOSEMA HAPANA (WATU 80)
70% Walidai kuwa, hawakwenda kuhakiki kwenye daftari la mpiga kura.
21% Walidai kuwa, kupiga kura ni kujisumbua na kupoteza muda. Yeyote atakaye chaguliwa ni sawa.
9% Hawa kuwa na sababu maalumu.
........... MWISHO..........
ZINGATIA.
Utafiti wangu haukujikita kwenye chama chochote cha siasa.