Ndugu Kibosile Msemakweli, Mtanzania wa kwanza kwenda mwezini

iamwangdamin

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
864
Reaction score
1,798
Wanasayansi wa anga kutoka Tanzania wanatarajia kurusha chombo kinachoitwa HAPA KAZI TU SPACE ROCKET kwenda mwezini kikiwa na Mtanzania mmoja kwenda kufanya uchunguzi na kutembelea mwezi mnamo mwezi ujao.

Waziri wa Uchukuzi kamkabidhi funguo Ndugu Kibosile Msemakweli ili aweze kuwasha chombo hicho na kupiga usukani kuelekea mwezini, kama mdau wa sayansi na mambo ya anga napenda kutoa pongezi kwa taifa kufikia hatua hii, wadau mbalimbali kutoka jamii ya wana anga kama NASA nk wamepongeza juhudi za TANZANIA kuweza kufanikisha na kuwa kati ya pekee kutoka Afrika mashariki kufanya kitu kama hiki.

Chombo hicho kitasafiri kwa mwendo kasi sana na kitarushwa kutokea uwanja wa taifa, wananchi wa Temeke wasiogope wakadhani kambi ya Mbagala imelipuka tena kwa moto wa roketi hiyo wakiona, kingine wamesema chombo hicho kitakuwa na kila kitu.

Mihogo ya miezi miwili washamchemshia Ndugu Kibosile ili asife njaa. Ataondoka na panadol za kutosha pia.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Hii itakuwa taarifa ya faraja sana kwa wale ndugu wazalendo wana halisi wa awamu 5.

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!

Hiiiiii bagosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…