Ndugu Malisa GJ elewa kuwa SI UNIT ya uanaharakati ni Jela au Kifo. Ukisema unaogopa Kifo na hujui hatma ya Watoto wako ni kwamba hujui unachokifanya

Ndugu Malisa GJ elewa kuwa SI UNIT ya uanaharakati ni Jela au Kifo. Ukisema unaogopa Kifo na hujui hatma ya Watoto wako ni kwamba hujui unachokifanya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
NDUGU MALISA GJ ELEWA KUWA SI UNIT YA UANAHARAKATI NI JELA AU KIFO. UKISEMA UNAOGOPA KIFO NA HUJUI HATMA YA WATOTO WAKO. NI KWAMBA HUJUI UNACHOKIFANYA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nimeona àndiko la ndugu MALISA GJ akiwa anaonyesha Hofu yake kuhusiana na kupewa taarifa kuwa naye yupo kwèñye List ya Watu wanaotafutwa Kuuawa. Malisa amejaribu kueleza Hofu yake kuhusu nini kitatokea endapo akikutwa na wanyonya Roho, Wauaji, na wakafanikiwa kumuua. Watoto wake NI wadogo itakuwaje?

Malisa, kufa Mtu anaweza kufa Wakati wowote ule Bila kujali unamtoto au Hana, Bila kujali Watoto wake Wanaumri mdogo au Mkubwa. Kufa kupo tuu. So suala la wewe kufikiri ukifa nini kitatokea Hilo achana nalo.

Uanaharakati hasa wa kutetea HAKI lazima kîla Mtu ajue SI UNIT yake ni KIFO na wale weñye bahati huishia kufungwa Jela huku Wengine wakiishia kuwa walemavu.

Unapoingia kwèñye fani yoyote lazima ujue matokeo ya fani Husika.

Kazi ya uanaharakati sio Kazi ya kichungaji au sheikhe. NI Kazi zaidi ya uchungaji na usheikhe.
Nafahamu wàpo wachungaji na masheikhe àmbao nao NI wanaharakati àmbapo watabeba wajibu wa kichungaji/kisheikhe na hapohapo wajibu wa kianaharakati.

Unapokuwa mwanaharakati NI tangazo rasmi kuwa umejikana Nafsi na umejitoa Mhanga Maisha yako kwaajili ya Wengine. Kwako Kufa siô tatizo, ila tatizo kwako NI kutaka kuona Haki au Jambo unalolipigania linakamilika.

Uanaharakati ni Kazi ya kitume, Kazi ya kinabii. Kûna ethics, morals na standards Zake Ambazo mwanaharakati lazima awe nazo ili angalau aweze kudumu walau Kwa Muda mrefu huku Mungu akimuepushia na Mikono ya Adui Zake.

NI hatari kuwa mwanaharakati ukiwa na mrengo Fulani au Maslahi Fulani. Huo hauwezi kuwa uanaharakati.

1. Mfano, unakuwa mwanaharakati wa kutetea Waislam alafu Haki za Watu wa Dini zingine hauzitetei. Huo siô uanaharakati. Ila NI kwamba unafanya biashara Fulani àmbayo itakulipa Kwa sababu unatetea upande wako.

2. Unajiita mwanaharakati wa kutetea Waafrika, kisa wewe NI Muafrika badala ya kutetea HAKI za Watu wôte.

3. Uanaharakati wa kutetea Wanawake pekee huku ukiacha Haki za Wanaume. Huo siô uanaharakati.

4. Uanaharakati wa kutetea Chama Fulani cha siasa Ikiwa wewe NI mwanachama wa chama Huko.
Mfano, unakuwa CCM alafu unajiita mwanaharakati wa Haki za binadamu alafu kwèñye hizô Haki unatetea CCM huku kwingine hakukuhusu.

Yàani kutetea linalokuhusu alafu lisilokuhusu àmbalo NI Jambo lilelile wewe Huna habari nalo.

Wanaharakati Kamili, hawapaswi kuwa na maslahi ya upande wowote isipokuwa kutetea kile kinachoitwa HAKI.

Kwa mfano, mwanaharakati hataangalia kama aliyefanya Jambo Fulani baya NI Nani hata angekuwa yeye au Mzazi wake au Mtu yeyote lazima awajibike.

Jina la Yuda, ni Moja ya Majina maarufu katika ulimwengu wa kiyahudi na Wakristo. Legacy pekee àmbayo Yuda mwenye jina lake aliacha ni kuweza kuwajibika. Uanaharakati wa kuhakikisha Haki inatendeka.

Uanaharakati ni uwezo wa kupigania Haki, yàani kuweza kuhukumu na kujihukumu Kwa kweli yôte.

Siô akifanya huyu Kimya, akifanya Mwingine Kelele. Hizô siô Harakati. Bali huitwa Siasa.

Uanaharakati ni ule uwezo wa kuweza kujikosoa au kukosoa Eneo àmbalo wewe mwenyewe upo.
Mathalani, ukiwa CHADEMA úwe na uwezo wa kukosoa CHADEMA kama vile àmbavyo ungekosoa CCM au Chama kingine ambacho wewe siô Memba.

Tundu Lisu kipande Hiki anafanya Vizuri. Lisu unaweza muita mwanaharakati. Kwa sababu anauwezo siô tuu WA kukosoa CCM Bali hata kuikosoa CHADEMA Mpaka kufikia Watu wanasema anagombana Mwenyekiti Mbowe.

Msimamo wa LISU upo kianaharakati kwamba yeye hata CHADEMA anaweza kuondoka Muda wowote endapo mambo yakibadilika.

Mwanaharakati hapaswi kuogopa KIFO Wala JELA.
Ila lazima ajue kujihami na kukimbia kama itawezekana. Yàani kujilinda.

Ukishakuwa mpigania HAKI NI dhambi kûbwa kuomba hisani Kwa Mtu àmbaye ulikuwa unamsema anafanya dhulma.

Yàani HAKI kujisalimisha kwèñye dhulma.
Yàani kumpigia Magoti Shetani au kumwomba Msamaha Shetani.

Mwanaharakati hawezi kumwomba Shetani Msamaha.
Option atakayompa Shetani ni Mbili tuu:
1. Kumwambia abadilike awe Mwema.
2. Kumwambia Afanye atakavyoweza lakini Kamwe hatofuata masharti yoyote Kutoka Kwa Shetani

Malisa, NI hatari kuingia kwèñye uanaharakati ukiwa unajua unaipenda familia yako kuliko kile unachokifanya yàani kutetea Watu au HAKI.
Matokeo Yake ni kujilaumu na Kazi yako itakuwa Sawa na bure Kabisa.

Mwanaharakati lazima ajijenge kwèñye kipengele cha HAKI na Haki NI malipo anayostahili Mtu. Malipo hayo huitwa Majina mengi lakini jina maarufu huitwa KISASI.

Kisasi ni Malipo ya Mtu aliyeonewa au kudhulumiwa àmbaye hakupewa Haki yake Kwa utaratibu uliowekwa. Yani utaratibu ulikiukwa.

Utaratibu uliokiukwa kimakusudi katika kumpa Mtu HAKI yake ndîo huitwa KISASI. NA Kisasi hakinaga neno MSAMAHA.
Msamaha ni Nafasi ya pili anayopewa mkosaji, mdhulumaji, muonevu Ikiwa atajirudi Kwa Wakati.
Mtu asipojirudi Kwa Wakati íwe Kwa sababu yoyote Ile íwe kusahau, kutokujua, kiburi au dharau Kisasi huwa Halali kwàke.

Mfano, Mtu hawezi akauawa Hapo alafu MTU Mwingine asiyehusika akasema aliyeua asamehewe.
Kisasi lazima kilipwe.

Harakati lazima ziseme HAKI yôte na kweli yôte Bila kuacha hata nukta Moja.

Watoto wa wanaharakati wale halisi wôte hufundishwa HAKI. Kisasi ni Moja ya Nguzo za HAKI.
Bila Kisasi Huwezi kujiweka kwèñye Nafasi ya Watu weñye HAKI.

NI jukumu la wanaharakati Kuoa wake au kuolewa na Wanaume wanaojua maana ya HAKI. Kisha Watoto nao automatically wataijua Haki. NI jukumu la Watoto au wajukuu kulipa KISASI Ikiwa kûna mambo yalienda ndivyo sivyo kimakusudi Kabisa.

MSAMAHA ni neno ambalo weñye dhulma hulipenda kulitumia vibaya na hii hufanya maovu yazidi kuongezeka na Watu kuzidi kuonewa.

Watibeli tunajua weñye Haki watalipwa na weñye Haki.
Kwa kipimo kilekile.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam

Pia soma: Godlisten Malisa: Nimetajwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kuuawa, naishi kwa hofu, sijui hatma ya watoto wangu
 
Back
Top Bottom