Kama ambavyo imefanyika kwa ugonjwa wa Malaria siku ya Jumamosi (13/02/2010), tunaomba na kupendekeza pia matatizo haya makubwa katika taifa letu nayo yatanganzwe rasmi kama majanga ya kitaifa:-
1. Uduni wa ufahamu wa Wakulima wetu katika matumizi ya mbegu bora, mbolea na ukulima wa kisasa.
2. Uhaba wa KUTISHA wa Madawati katika shule zetu za msingi na sekondari. Ni aibu kubwa kwa watoto wetu kusoma wakiwa wamekaa chini
3. Uhaba mkubwa wa vitabu toka ngazi ya shule za msingi mpaka chuo kikuu
4. Ufaulu duni na usiokubalika wa Wanafunzi wetu katika masomo ya Hisabati na Sayansi
5. Uhaba wa walimu bora hasa kwa masomo ya Hisabati na Sayansi kwa shule za msingi na sekondari.
6. Mamilioni ya Watanzania wenzetu wasio na ujuzi na utalaam wowote ambao ni muhimu sana katika kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuboresha maisha yao