Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Anaandika rafiki yake na SATIVA 🧵 Taivina James ✍️
Nilitaka niandike baada ya kuona upande wetu ambao ni wa familia ni nini kitafanyika baada ya Statement ya jana lakini bado kimya. Acha niongee kwa upande wangu mwenyewe iko hivi Sativa alipotea kwa siku zaidi ya 3 mimi ndo mtu wa kwanza kugundua kuwa Sativa amepotea na ndio mtu wa kwanza kutoa taarifa na kuomba msaada mitandaoni kuwa Sativa kapotea.
Mungu mkubwa wanafamilia wa X na walio nje ya X walifanikisha kumpata Sativa akiwa majeruhi sana. Akiwa katika maumivu makali hao hao wanafamilia wetu walihakikisha Sativa anakuwa salama kwa kuanza kuchanga pesa za matibabu na msaada usiohitaji pesa pia wanafamilia wa X na wa nje pia walisaidia kupatikana kwake. Wakati Sativa anasafirishwa kuja Dar kuna Back up ya Polisi ambayo alipewa haikuwa bure Gharama zilitumika na gharama zilizotumika ni hizi hizi walizo changa wana X.
Amepelekwa Hospital Sativa amepata Msaada kutoka sehemu tofauti tofauti likiwepo shirika la kina wakili Kisabo ni Upendo mkubwa sana. Hivo mnaweza mkakubaliana na mimi kuwa upande wa matibabu na gharama zake Familia ya X na nje ya X wameweza na wanaweza pia kupambania mpaka Sativa apone hata kama zitajitajika zaidi wapo tayari kuchanga.
Kuna miamala ambayo ilikuwa ikirudishwa ile miamala ilirudishwa kwasababu ambao walitoa baada ya kupatikana kwa Sativa hawakuonyesha ushirikiano kipindi anatafutwa hivo walirudishiwa hela zao kwa macho yangu nilishuhudia watu wakituma hadi Tsh 100 kuhakikisha Sativa anakuwa salama kifupi watu wa X na nje ya X wangeweza kufanikisha kila kitu ambacho kinahitajika kwa Sativa wameshindwa sehemu moja tu nayo ni kuwawajibisha watu waliohusika na tukio la Sativa.
Jambo hilo hawawezi kufanikisha bila Serikali na vyombo vya Dola. Binafsi naamini wananchi tunahitaji serikali iwawajibishe wote waliohusika na tukio la utekaji wa Sativa wala sio kutoa msaada wa ki fedha kwa mhusika. Kama Familia ya X na wengine wamefanikisha kuhusu matibabu basi sioni haja ya serikali kuanza na msaada wa matibabu nadhani msaada mkubwa ambao tunahitaji ni Wahusika kuwajibishwa.
Kwanini watu wanatekwa kila siku wengine hawana sauti mitandaoni kama alivopigiwa kelele Sativa hivo wanapotea mazima.
Kiufupi msaada unaohitajika kwa Serikali ni kupata mrejesho wa kisheria kuhusu waliohusika ili wengine wajiskie salama zaidi katika nchi yao kama serikali ingehitaji kutoa msaada ingeanzia kwanzia siku ya kupotea kwake kupatikana kwake na usalama wake lakini hata polisi ambao walitoa back up ya Sativa kuja Dar walilipwa na hela zilitoka kwa familia ya X na nje ya X.
Utamsaidia Sativa matibabu atapona watekaji bado wapo wataendelea kuteka wengine utasaidia matibabu ya wangapi? Kwanini tusionyeshe funzo kwa watekaji ili kuepuka gharama za kuhudumia watu wengine ambao wanatekwa.
Binafsi kama upande wetu ambao ni upande wa familia kama utabariki hiki kinachoendelea mimi binafsi ntajitoa kwenye kila kitu kinachohusiana na ndugu yangu ntaishia kwenda kumuangalia kama Stranger.
Kwa upande wangu kukubaliana na hilo swala ni kuwa Disrespect watu waliojinyima kula na kuchangia matibabu ya Sativa na ni usaliti na usaliti sio kitu kizuri.
HAKI ITENDEKE KWANZA KWA MANUFAA YA WENGINE
Pia soma Kuelekea 2025 - Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa hadi apone, aagiza uchunguzi wa tukio hilo