Ndugu yangu amefukuzwa kazi kisa fao la kujitoa

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
56,205
Reaction score
79,515
Umofia kwenu wana JF,

Ndugu yangu ambaye alikuwa anafanya kazi softnet amefukuzwa kazi kwa sababu alichukua fedha zake za NSSF wakati bado anaendelea na kazi.

Amekuja kuomba Ushauri kama wanasheria wanaweza kumtetea na kupata haki yake.

Swali aliloniuliza kama kuchukua fedha NSSF ni kosa kisheria mbona mifuko mingine unaweza kuchukua hata nusu ya mafao huku ukiendelea na kazi?

Yupo home Arusha amekuja kupunguza machungu na kuwaona ma advocates wa huku.
 
Mimi sio mwanasheria but kama fao linasema ulete barua ya kuachishwa kazi
ili upewe na ndugu yako alipeleka hiyo barua basi kafukuzwa kwa forgery
 
Kama ali foji barua ya kuachishwa kazi hawezi saidika, ila swali lingene la kujiuliza nani kapeleka izo information kazini kwake,
 
Mimi sio mwanasheria but kama fao linasema ulete barua ya kuachishwa kazi
ili upewe na ndugu yako alipeleka hiyo barua basi kafukuzwa kwa forgery

Ni kweli ameniambia amefanya magumashi hayo,Ila concern yake kwanini afukuzwe wakati fedha ni zake? kwani mtu si anaweza akaterminate contract halafu akasign nyingine kwanini softnet/nssf wasichukulie kwa minajili Hiyo maana fedha ni zake.
 
Ishu sio fedha zake au la
ishu ni kuwa hulipwi mafao bila kupeleka barua ya muajiri
na kama muajiri hakukupa na wewe uka forge yako
muajiri amemfukuza kwa kosa la kufanya forgery na sio kuchukua fedha
 
Mimi si mwanasheria ila kama alipeleka barua ya kuacha kazi NSSF basi hapo hakuna msaada wowote ukizingatia akienda mble zaidi yeye ana makosa ya kugushi; kwanza, baru ya kuacha kazi, pili, hati/sahihi ya mwajiri wake pamoja na muhuri ya ofisi anayofanya kazi
 
Kama ali foji barua ya kuachishwa kazi hawezi saidika, ila swali lingene la kujiuliza nani kapeleka izo information kazini kwake,

Anadai Mifuko imestukia kwamba watu wanachukua fedha kimagumashi hivyo ukipeleka barua ya kuacha kazi mifuko inakuja direct ofisini kwako kuuliza alichokosea amasema hr alikuwa hajui so nssf wakailazimisha ofisi imchukulie hatua.
 
hilo ndo jibu
hakuna cha kumsaidia
 
Ishu sio fedha zake au la
ishu ni kuwa hulipwi mafao bila kupeleka barua ya muajiri
na kama muajiri hakukupa na wewe uka forge yako
muajiri amemfukuza kwa kosa la kufanya forgery na sio kuchukua fedha

Ok Thanks wadau ngoja nimfahamishe Ila jamaa kachanganyikiwa anaona Kama ameonewa.
 
Ni kweli ameniambia amefanya magumashi hayo,Ila concern yake kwanini afukuzwe wakati fedha ni zake? kwani mtu si anaweza akaterminate contract halafu akasign nyingine kwanini softnet/nssf wasichukulie kwa minajili Hiyo maana fedha ni zake.

Bora atulie, kwanza NSSF/mwajiri wake anaweza kumshtaki kwa forgery...
 
Watu wengine bwana unafoji na umenusurika na kesi ya jinai ya kughushi bado unadai hujui kosa!
 
huyo muhuni. Fao la kujitoa unachukua ukiwa umeresign. Huo huwa ni ujanja unafanya na alijua risk yake.

mwambie ataliwa pesa yake bure. Anatakiwa akamatwe kwa kuforge nyaraka maana lazima awe na barua ya kuacha kazi ili achukue hizo pesa.
 
Ni kweli ameniambia amefanya magumashi hayo,Ila concern yake kwanini afukuzwe wakati fedha ni zake? kwani mtu si anaweza akaterminate contract halafu akasign nyingine kwanini softnet/nssf wasichukulie kwa minajili Hiyo maana fedha ni zake.
Ni mwizi ameiba signature na mihuri ya kampuni.
Hawezi kusaidika.
Atafute shughuli ingine
 
Navyofahamu mimi, mafao hayo hutolewa pindi mtu anapoachishwa au kuacha kazi. Na barua ya kuacha/kuachishwa kazi inatoka kwa muajiri, na hata baadhi ya vipengele vya kwenye fomu za kuchukuliwa hayo mafao yako inabidi yajazwe na kuthibitishwa na muajiri. Sasa yeye ilikuwaje akachuka hayo mafao angali bado muajiriwa? Kwa maana ni kwamba alifoji taarifa. Kama alifoji basi hilo ni kosa la kutoonesha uaminifi kwa mwajiri wako ndiyo maana amefukuzwa. Kama kaweza kufoji mafao yake maana yake kwamba siku atafoji kabisa kampuni nzima na kuwa yake.
 
Some create their own storms and get mad when it rains.

Hao wanasheria ni kama waganga wa kienyeji tu,hawakuambia kama kesi yako huchomoki,watamlia hela na atajikuta ana kesi ya kughushi nyaraka.

"At last it's the client's case" hapo wakishakulia hela ndo wanaambizana.
 
hayo mafao kachukuaje bila management kujua/utaratibu ni lazima mwajiri ajaze fomu ya nssf aweke sahihi na muhuri sasa,lakini pia kabla hujaanza hatua yeyote ya kuprocess mafao ni lazima uende na barua ya mwajiri ikikuonesha ama umeacha,kuachishwa au kustaafu kazi.sasa sijui huyo ndugu yako alifikiaje hayo mafao nnje ya taratibu.muhimu kupita vyote ni kuwa nssf hawana fao la kujitoa.
 
Ni kweli ameniambia amefanya magumashi hayo,Ila concern yake kwanini afukuzwe wakati fedha ni zake? kwani mtu si anaweza akaterminate contract halafu akasign nyingine kwanini softnet/nssf wasichukulie kwa minajili Hiyo maana fedha ni zake.

shida ni ameforge barua..yani hapo ni kesi na muajiri angeshinda, wala asilalamike, ashukuru Mungu tu hawajamuamulia kivingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…