Ndugu yangu amepata msongo wa mawazo (depression)

Upendo iswa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
345
Reaction score
548
Habar za mchana wakuu,

Ndugu yangu ( me) amepata msongo wa mawazo na tumejaribu kumsaidia kisaikolojia, alipata nafuu kwa muda, ila hali imejirudia tena.

Mbinu gani nitakazotumia aweze kujirudi katika hali yake ya kawaida.

hili tatizo limerudi leo ni siku ya tatu anakuwa mnyonge sana hajiamini na anapenda kukaa peke yake. Kabla ya ugonjwa alikuwa hana tabia ya kujitenga hivi.

Naombeni msaada wa kimawazo wakuu
 
Akitaka kupona aamue kumpokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha na kuamua kuishi maisha safi ya kiroho; kama hawezi aamue kujipenda mwenyewe na mazingira na watu wanaomzunguka watu wanaomkosoa aachane nao kabisa huku akiendelea kukaa na watu wanaomkubali na akiendela kujiaminisha moyoni yeye yupo vizuri kwenye kila kitu huku akiangalia zaidi strength zake kuliko weaknes
 
Chanzo tumekijua kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti flani...sasa huyo binti akamuacha
Kama chanzo ni mapenzi,

Huyo hakuna tiba kwake, wala usijisumbue, hata apikiwe chakula anachopenda na mama yake mzazi, hazinduki!!!. Ila usiwe na wasiwasi, atapona tu. Mpeni muda wa mwezi mmoja au mwezi na nusu akae na kujitafakari kwa utulivu bila kumkera kera hovyo (mkimkera na kumsumbua sana mnamuongezea mawazo, na anaweza kufanya maamuzi mabaya zaidi).

Hua inatokea kwa sisi wanaume, katika hatua fulani ya maisha, pindi unapotokea kukamatwa maskio na mwanamke, hufurukuti wala huruki kwake, halafu akakuacha kwa ghafla/bila sababu maalum, ila baada ya muda yanasahaulika na maisha kuendelea mbele. Athari hua inakua kubwa kama HAUNA AJIRA ya kukufanya uwe bussy.

ILAAAAAA, kawaida mtu kama huyo akipona huo msongo wa mawazo ya mapenzi na kurudi katika hali yake ya kawaida, hua wanajiwekea KIAPO MAALUM cha kuwanyoosha wanawake, wanawake hua wanatikiwa wajiandae na wafunge mkanda kwa wanaume kama hao (mtaani kwenu watamkoma). Atakua kama jasusi lenye ROHO ya chuma, ni kuwapanga mstari na kugegeda halafu kusepa, NO LOVE STORY kwake. (Imeshanitokea mimi binafsi na rafiki yangu hio hali).
 
Asante. Huyu ndugu yangu hajiamini, ( amekuwa na law self esteem)
 
Kama hajaamua kumove on itakuwaje sasa maana amekuwa kama amechanganyikiwa
 
kwanza tambua chanzo cha ugonjwa huo pili jaribu kukaa nae na kumdadisi pia mtembeze sehemu ambazo anaweza kufurahi na mengineo
 
Ana umri gani? Wakati fulani hupaswi kushauri kuzidi uelewa wa mtu. Kwakuwa simfahamu, umri wake unaweza ukanipa picha ya yeye ni mtu wa aina gani na ni ushauri gani utamfaa
 
Ana umri gani? Wakati fulani hupaswi kushauri kuzidi uelewa wa mtu. Kwakuwa simfahamu, umri wake unaweza ukanipa picha ya yeye ni mtu wa aina gani na ni ushauri gani utamfaa
mkubwa mzima ww mpaka mtu akawe na msongo wa mawazo bado huyo no mtoto? sometimes unatakiwa kujiongeza
 
mkubwa mzima ww mpaka mtu akawe na msongo wa mawazo bado huyo no mtoto? sometimes unatakiwa kujiongeza
Namna anavyo himili msongo wa mawazo mtu wa miaka 10's ni tofauti na 30's na pia ni tofauti na 40's. Na ndio maana hutakaa usikie mzee wa miaka 60 amejinyonga kisa kaachwa na mke au kimada.
 
Namna anavyo himili msongo wa mawazo mtu wa miaka 10's ni tofauti na 30's na pia ni tofauti na 40's. Na ndio maana hutakaa usikie mzee wa miaka 60 amejinyonga kisa kaachwa na mke au kimada.
mtu wa miaka 10 hawez kuwa na msongo wa mawazo wa kimapenz hata siku moja
 
'hua wanajiwekea KIAPO MAALUM cha kuwanyoosha wanawake, wanawake hua wanatakiwa wajiandae na wafunge mkanda kwa wanaume kama hao (mtaani kwenu watamkoma). Atakua kama jasusi lenye ROHO ya chuma, ni kuwapanga mstari na kugegeda halafu kusepa, NO LOVE STORY kwake. (Imeshanitokea mimi binafsi na rafiki yangu hio hali)'.Umenikumbusha jambo,nilikuwa nina rafiki yangu alikuwa ni mtu wa aina hiyo,kuchukua na kuacha,haijalishi mwanamke ni mzuri au mbaya,nilipo anza kumchunguza kwanini amekuwa na hii tabia niligundua kuwa aliwahi kutendwa na mwanamke ambaye alikuwa akimpenda sana baada ya kumfumania na mwanamke...
 
Chanzo tumekijua kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti flani...sasa huyo binti akamuacha

Hihihi,huyo jamaa wa wapi huyo,watu tumeachwa hadi balaa na hatuna depression,ndio kabalehe juzi juzi nini huyo ndugu yako,mwangalie kwa makini asije kujinyonga
 
Ana umri gani? Wakati fulani hupaswi kushauri kuzidi uelewa wa mtu. Kwakuwa simfahamu, umri wake unaweza ukanipa picha ya yeye ni mtu wa aina gani na ni ushauri gani utamfaa
Ana umri miaka 23 bado ni kijana mdogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…