A
Anonymous
Guest
MALALAMIKO KUTOKA FAMILIA YA MAREHEMU WOLFGANG M.TURUKA.
Tangu tarehe 14/9/2020 ndugu yetu Tito hajulikani alipo na familia tunazo taarifa kwamba Polisi walimpiga akiwa kituoni na kumuua, kisha wakamzika kusiko julikana.
Ofisi ya RPC Ruvuma walifungua jalada la uchunguzi tangu tar. 28/2/2024 mpaka leo wamekaa kimya na hatujui hatima ya ndugu yetu.
Kinachosikitisha zaidi ni kutopata ushirikiano na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga ambaye barua yetu tulimwandikia kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ila sasa hata simu zetu hapokei.
Tunaiomba Serikali ambayo inajukumu la kulinda uhai wa watu wake, kupitia ngazi na vyombo vinavyohusika akiwemo Mh. Waziri Mkuu, Mbunge pamoja na Mh. Waziri wa Mambo ya Ndani, kwamba sisi familia tunataka kumpata ndugu yetu; tunaomba wamrudishe akiwa hai au maiti yake, na familia tupate haki ya kumzika ndugu yetu.
Tunaziomba asasi na vyombo huru vya habari vitusaidie kupaza sauti ili ndugu yetu Tito Wolfgang Turuka apatikane."