Dah! Wakuu hii ndiyo hali halisi ya Watanzania wengi. Suala la kuangalia sura za wenye mambo safi kwenye blog na magezeti zinatufanya tusahau taswira halisi za ndugu zetu. Wakuu mlioleta picha kula tano, kudos.
Jamani madhara ya umasikini na ujinga ni makubwa sana. Watu hawa hawana mlo bora, usafi kwao ni tatizo na maradhi kama vile kuoza meno, ugonjwa wa ngozi hayakosekani.
Hapa ujinga nimeuweka kwa maana ya kwamba usafi haufungamani sana na umasikini. Unaweza kuwa masikini sana bado ukajitahidi kuwa msafi. Turudi kwenye vita iliyotangazwa na baba wa Taifa dhidi ya ujinga, umasikini na maradhi.