Asante sana mkuu,, tylodox niliwapa wakubwa Ila wadogo niliambiwa niwape extratetracycline ila naona bado tatizo lipo mkuu1.Nianze na vifaranga kusinzia na kutoa machozi hizo ni dalili za mafua....chunguza pia dalili hizi kujithibitishia uwepo wa ugonjwa wa mafua
a. Ute ute mdomoni
b.mafua puani
c.kupumua kwa shida/kukoroma
d.kupiga chafya
e.mabawa kuchafuka kwasababu ya kuku kupangusa uchafu wa machoni maana huwa unawasha.
Wape kuku wako dawa ya mafua kwa muda wa siku 5...wanywe maji ya dawa tu.
Tumia Limoxin au Tylodox kuwatibu....Ukikosa mojawapo kati ya hizo unaweza kutumia Ganadex au Enrovet.
Asante
Asante Sana mkuu,, dalili ulizozitaja za NDUI naona zote wanazo na pia sijawahi kuwachanja chanjo ya NDUIKuvimba kwa macho kunaweza kusababishwa na mafua.....ila kesi ya mafua katika macho ndani yanakuwa na uchafu mweupe kama sabuni iliyolowa.....
Ninachokiona kwenye hizo picha ni NDUI...
JE KUKU WAKO ULIWACHANJA NDUI?
NDUI DALILI ZAKE
NI KUVIMBA USO
KUKU ANAPATA VIDONDA SEHEMU ZA USONI
UPANGA MACHO PUA VINAATHIRIKA NA SEHEMU ZA WAZI AMBAZO HAZINA MANYOA
VIDONDA VINAKUWA NA MADOA MEUSI MITHILI YA KUUNGUA KWA MOTO
Kama hukuwachanja ndui usitoe chanjo ugonjwa ukishaingia bandani kwako au maeneo jirani subiri ugonjwa uishe.
Fanya yafuatayo
Osha vidonda kwa maji ya chumvi na uwapake Iodine au mafuta ya mboga
Wape OTC kupunguza ukali wa ugonjwa
Yaani mpaka Mimi mwenyewe naanza kuhisi ni bora uwaachie, maana kuku wa majirani wanaoachiwa wenyewe wako poa tuu Ila wa kwangu ninaowaweka bandani ndio tatizo limewakumbaDah ufugaji wa kuku wa kienyeji unataka ujasiri sana,nilichogundua kwa uzoefu ni bora uwaache wazurure wanakuwa salama kuliko ukiwafungia kwenye banda,wanaugua sana...
npo pamoja na wewe, hasa kama upo sehem ambayo huingilian na watu wengine n vyema wazulule japo risk n kubwa,Dah ufugaji wa kuku wa kienyeji unataka ujasiri sana,nilichogundua kwa uzoefu ni bora uwaache wazurure wanakuwa salama kuliko ukiwafungia kwenye banda,wanaugua sana...