Ndugu zangu wa mikoani tushirikiane kutimiza wazo langu la biashara

Ndugu zangu wa mikoani tushirikiane kutimiza wazo langu la biashara

Joined
Aug 15, 2024
Posts
49
Reaction score
72
Awali ya yote, Nashukuru Sana kwa kutenga muda wako na kupitia Uzi huu.

Leo nimepata wazo la biashara linalohusiana na kutoa huduma kwa watu mbalimbali hasa wa mikoani na wale wote ambao wapo nje ya jiji la Dar es salaam.

Nimepitia Nyuzi nyingi na mitandao mingi ya kijamii kwa muda mrefu sasa,nikapata muda wa kuona wapi panachangamoto gani na pafanyike nini japo nilikosa mda mzuri wa kuliweka Sawa hili wazi na hii inatokana na kuwa muda mwingi nilikuwa Niki focus na elimu.

CHANGAMOTO NILIZOZIONA;

1. Ugumu wa ufikiaji wa bidhaa kwa watu wa mikoani, hasa wanapozitaka kutoka Dar.
2. Gharama za ufatiliaji endao itawalazimu kuja kuchukua mizigo.
3. Umbali, ambao hufany kushndwa kuziacha biashara kuja Dar.
4. Ufinyu wa kutokulijua jiji vyema hususani machimbo ya bidhaa.
5. Kutokuwepo kwa uaminifu baina ya wafanya biashara wa mikoani na maduka ya mtandaoni.
6. Upotevu wa muda mwingi kwa mtu mmoja kufuatilia kilakitu( uagizwaji,ununuzi,kutafuta chimbo) nk.

WAZO NILILOPATA BAADA YA KU STUDY HIZO CHANGAMOTO.

1. Kuwa mtu ambaye sio winga, utaniagiza bidhaa yeyote iwe duka unalolifahamu au laa kisha utanunua bei ya dukani kwa kukubaliana na mwenye duka na malipo mtafanya bila Mimi kuhusuka na chochote.
2. Nitasimamia huo mzigo wako process zote hadi kutumwa huko uliko. Kama pia Una chain yako ya usafirishaji ambayo huwa unatumia kampuni Fulani ni njema zaid.
3. Lakini pia utanituma kufuatilia details zozote za kibiashara, ikiwemo unasehemu umesikia kuna ABC unataka kuhakiki km Hilo duka lipo na bidhaa zipo basi Mimi nipo kwaajili yako huna haja ya kufunga safari
4. Kama haitoshi, Nita act km personal assistant wako kweny kukuwakilisha kimanunuzi yoyote nikiwa Dar wewe ukiwa mkoani kwani elimu ipo japo sio kubwa ila ninaujuzi wa Kati katika MARKETING hivyo ninajua ninachoongea.

MALIPO
Malipo yatakuwa ni madogo Sana Sana Sana kulingana na huduma husika na namna tutayokubaliana na mteja wangu, niwatoe hofu tena bei itakuwa Sawa na bure na utalipa baada ya process mzima kukamilika.

PENDEKEZO
Kama ipo namna yyte na kurasimisha kisheria hii naomba wajuzi mnipe elimu, nipotayari kufuata tarajibu ili kuongeza uaminifu zaidi, na km haipo basi nikoradhi kuweka wazi nyaraka yoyote stahiki ili kuongeza uaminifu na kuonesha Nia yangu ya dhati katika kutoa huduma hii.

Napokea ushauri pia wa Aina yoyote ili kuboresha wazo langu.

Asante🤝
 
Wazo ambalo halitekelezeki kirahisi, mpaka mtu anatuma pesa za malipo Kwa mwenye duka bila wewe kuhusika Ina maana ana uhakika na mahali anaponunua bidhaa zake na ofisi zao anajua zilipo....



Ofisi/maduka karibu yote yanaouza bidhaa yana huduma ya kumtumia mteja wake bidhaa hata akiwa mkoani



Mzigo usipofika Kwa mhusika office/duka linakua accountable...


Sasa wewe ukichukua mzigo wa mtu alafu usipofika tuseme hata kampuni ya usafirishaji wakaupotezea, nani atakua accountable hapo??
 
Yah! Ni kweli mkuu. Ila nikisema Mimi sihusiki na chochote kwenye manunuzi nakuwa nime base upande wa malipo. Watu wengi unaowaona wanaposti bidhaa online hizo biashara co zao. Wengi ni mawinga ambao inabidi umpatie pesa kwa bei mliyoongea ndipo akate cha juu. Hivyo basi kwangu itakuwa tofauti nikimaanisha Mimi sitokupangia bei na hela yako hutonipa Mimi Bali nitakusanya huo mzigo duka husika wakati nimeshakuunganisha na mwenye duka muongee.

LENGO NI KUONGEZA UHAKIKA WA HUDUMA NA USALAMA WA BIDHAA.

Ukichunguza mitandaon utakuta account nyingi Sana zinapostiwa kutuhumiwa mtu huyo ametapeli watu akidai anaduka kariakoo kumbe mhuni tu.

Lakini pia, hizi tarajibu zote huwa zinaambatana na risiti, kwa mantiki hiyo hakuna namna ya kampuni ya usafirishaji kuruka hii dhamana kwakuwa risiti ina full details ya mzigo uliokwenda kinyume hivyo watawajibishwa na mamlaka.

Kama haitoshi, maduka mengi unayodai wanatuma mikoani huwa si maduka ni mawinga, utofauti wangu mimi na wao ni kuwa mimi nataka iwe rasmi, nitambulike na kuaminiwa kwa utaratibu mzuri na wateja na wauza wa jumla hii itaongeza confidence ya wanunuzi tofauti na kufanya kazi na mtu asiyefahamika kosa ambalo lolote linaweza kutokea bila mnunuzi kusaidiwa, mambo ambayo tunayasikia kilakikicha mitandaoni yakilalamikiwa.
Wazo ambalo halitekelezeki kirahisi, mpaka mtu anatuma pesa za malipo Kwa mwenye duka bila wewe kuhusika Ina maana ana uhakika na mahali anaponunua bidhaa zake na ofisi zao anajua zilipo....



Ofisi/maduka karibu yote yanaouza bidhaa yana huduma ya kumtumia mteja wake bidhaa hata akiwa mkoani



Mzigo usipofika Kwa mhusika office/duka linakua accountable...


Sasa wewe ukichukua mzigo wa mtu alafu usipofika tuseme hata kampuni ya usafirishaji wakaupotezea, nani atakua accountable hapo?
 
1738564139756logo.jpg.png

Mawazo 114 ya Biashara na Mitaji yake: Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuanzisha Biashara 114.
Whatsapp: 0687746471
 
Back
Top Bottom