Ndugu zangu Wasabato leteni ushahidi wenu kamili unaojitosheleza na kuthibitisha Jumamosi mnayopumzika leo ndiyo ya sabato halisi ya kwenye torati?

Wadau hamjamboni nyote?

Nauliza nipate kujua, nipate ilimu na maarifa

Swali lijibiwe bila mihemuko au hisia au chuki au kutegemea ushahidi wa wengineo

Leteni ushahidi wenu Wasabato

Tafakuri ya kina kwa wenye hekima

Usiku mwema
“Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,”
‭‭Lk‬ ‭4‬:‭16‬-‭17‬ ‭SUV‬‬

“Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza; wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi? Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno. Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka.”
‭‭Mk‬ ‭16‬:‭1‬-‭6‬ ‭SUV‬‬

“Hata ikiisha kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato, akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu. Lakini Pilato akastaajabu, kwamba amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo.”
‭‭Mk‬ ‭15‬:‭42‬-‭44‬ ‭SUV‬‬

Haya mafungu yanajieleza
Ukitaka na historia ya ni wakati gani hasa early Christians walianza kuabudu siku ya jua pia nitakupa
 
Yesu Kama desturi yake Alitunza sabato Luka 4:16
Kitabu cha Marko 16:1-6 kwamba siku ya kwanza ya juma kibiblia yani Jumapili Yesu alifufuka ukihesabu siku ya Saba ni jumamosi.
Marko 15 :42-44 hii ni siku alipo sulibishwa ijumaa ikitajwa Kama maandalio ya sabato
Ikimaanisha kwamba siku inayofuata ni sabato.
Kuna mafungu mengi ya Biblia tuanzie hapo
 
Mkuu nimeuliza ushahidi wa siku Jumamosi hii ya leo na siyo ilotajwa kwa Biblia, elewa swali
 
Kwani biblia iliyoandikwa na RC huwa mnaiamini?
 
Kwani biblia iliyoandikwa na RC huwa mnaiamini?
Ukli ndio huo usikimbilie iliandikwa na waroma
Received text haikutoka kwa waroma ambapo imetafsriwa King James Version.
Vulgate bible ndiyo ya wakatolic iliyochakachuliwa ili I support traditions nyingi za kipagani ziitwe ukristo pamoja na kubadili siku ya ibada ambayo wakristo wa mwanzo waliabudu on sabbath Saturday.

Mpaka 321 AD emperor Constantine alipogeuka kuwa mkristo aliwashawishi wakristo walioko Roma kwamba in order to convince waroma wawe wakristo tutumie siku yao ya kuabudu jua their supreme god maana walikuwa na miungu mingi lakini jua ndio supreme, ndio maana sunburst symbol iko kwenye makanisa Yao.
Na pia Sundays zikaanza kusherekea Kama siku ya Yesu kufufuka
Hivi ndivyo Sunday worship started badala ya sabato kinyume na Biblia inavyosema
 
Hata nisiende mbali

Kwann wanaosali jumapili wote, hamna anayejiita Msabato?.

Kwann tunaosali jumamos ,ndio tunajiiita wasabato ?.
 
Bila kushabikia ila katika kujifunza zaidi hata mimi nionyeshe wapi hapo jumamosi inaonekana sabato maana bado sijaona. Nilishaambiwa nisome mathayo 28 ila bado nikashindwa kuelewa.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Nauliza nipate kujua, nipate ilimu na maarifa

Swali lijibiwe bila mihemuko au hisia au chuki au kutegemea ushahidi wa wengineo

Leteni ushahidi wenu Wasabato

Tafakuri ya kina kwa wenye hekima

Usiku mwema
Ila sidhani kama itasaidia sana kwakuwa ni jambo linaloambatana na imani
 
Kwa hiyo ili tuende mbinguni ni lazima tuwe na siku ya kuabudu na siyo kumjua na kumtumikia MUNGU kila sekunde?
 
Nakubaliana na wewe; sabato ni Jumamosi maana wakibisha waulize kama Jumapili ni lini? Hiyo siku watakayosema ndiyo Jumapili basi waambie sabato ni siku ya kabla yake maana zafuatano. Ni suala la common sense tu. Muhimu zaidi ni wanaoabudu Jumamosi na wanaofanya hivyo Jumapili wote wako sahihi.
 
“If ye love me, keep my commandments.”
‭‭John‬ ‭14‬:‭15‬ ‭KJV‬‬
“Think not that I am come to destroy the law, or the prophets: I am not come to destroy, but to fulfil.”
‭‭Matthew‬ ‭5‬:‭17‬ ‭KJV‬‬

“And hereby we do know that we know him, if we keep his commandments. He that saith, I know him, and keepeth not his commandments, is a liar, and the truth is not in him. But whoso keepeth his word, in him verily is the love of God perfected: hereby know we that we are in him. He that saith he abideth in him ought himself also so to walk, even as he walked.”
‭‭1 John‬ ‭2‬:‭3‬-‭6‬ ‭KJV‬‬
Kama wakristo tunampenda Yesu lazima matendo yetu yaendane naye na kuzishika Amri kumi na ya nje inaanza kwa kusema remember Alijua binadamu wangejaribu kubadili.
Tukkikataa Amri ya nne ni kwamba tumevunja zote kutokana na Biblia
“For whosoever shall keep the whole law, and yet offend in one point, he is guilty of all. For he that said, Do not commit adultery, said also, Do not kill. Now if thou commit no adultery, yet if thou kill, thou art become a transgressor of the law. So speak ye, and so do, as they that shall be judged by the law of liberty.”
‭‭James‬ ‭2‬:‭10‬-‭12‬ ‭KJV‬‬
 
Hatutaokolewa kWa Amri kumi tunaokolewa kwa neema ya Yesu kristo pekee lakini tukisha ipokea neema na kumkubali Kristo Kama BWANA na mwokozi wetu , Tunatii Amri zake bila shuruti ikiwamo sabato.
Amri za Mungu ni 10 siyo tisa
 
Bila kushabikia ila katika kujifunza zaidi hata mimi nionyeshe wapi hapo jumamosi inaonekana sabato maana bado sijaona. Nilishaambiwa nisome mathayo 28 ila bado nikashindwa kuelewa.
Nimeshaandika hapo juu kwenye post zangu jinsi ya kutambua siku kitabu cha Marko 15 mpaka 16 siku aliyokufa Yesu tunajua ni ijumaa na Biblia inasema ni siku ya maandalio ya sabato,kwa hiyo siku inayofuata ni sabato ambayo ni jumamosi.
Pia siku aliyofufuka Yesu ni Jumapili Biblia inaisema kuwa ni siku ya kwanza ya juma kwa hiyo ukihesabu kuanzia Jumapili siku ya Saba ni jumamosi.
Asante
 
Kwa hiyo ili tuende mbinguni ni lazima tuwe na siku ya kuabudu na siyo kumjua na kumtumikia MUNGU kila sekunde?
Tunamuomba Mungu individually na collectively kila wakati,kila saa na kila siku
Kitu za Amri kumi za Mungu ni ushahidi kwamba tunamheshimu na kumuabudu
Katika Amri kumi sabato ni moja wapo huwezi ku pick and choose
Yakobo 2:10
“Here is the patience of the saints: here are they that keep the commandments of God, and the faith of Jesus.”
‭‭Revelation‬ ‭14‬:‭12‬ ‭KJV‬‬
“To the law and to the testimony: if they speak not according to this word, it is because there is no light in them.”
‭‭Isaiah‬ ‭8‬:‭20‬ ‭KJV‬‬
Huwezi kusema unampenda Yesu na unapinga Amri zake kuchagua zipi utunze zipi uache.
Barikiwa ndugu tunapoendelea kuchambua maandiko I am not better than you tunasoma tu kilichoandikwa ili tujue ukweli
Na Biblia ndiyo final authority kwa wakristo the received text siyo vulgate
 
Hatutaokolewa kWa Amri kumi tunaokolewa kwa neema ya Yesu kristo pekee lakini tukisha ipokea neema na kumkubali Kristo Kama BWANA na mwokozi wetu , Tunatii Amri zake bila shuruti ikiwamo sabato.
Amri za Mungu ni 10 siyo tisa
Kama Kristo asingalifufuka imani yetu ingalikuwa bure; ila Kristo amefufuka limbuko lao waliolala. Siku ile kukaja upepo kutoka mbinguni Roho Mtakatifu akawashukia wanafunzi siku ile ya Pentekoste kanisa la kwanza likazaliwa wakamwabudu Mungu katika roho na kweli.
 
Kwa hiyo unabishana na Yesu aliyekuwa ananyofoa masuke ya ngano na kuwaambia watu kwamba hajaja kuibatilisha torati bali kuikamilisha iwe bora kwa kuwaambia amri iliyo kuu ni UPENDO?
 
Kwenye hadithi nyingi za mtume muhammad(saw) zinathibitisha kuwa sabato ilikuwa jumamosi, siku baada ya ijumaaa
Wakati wa Yesu kulikuwa na siku zinaitwa Jumatatu,Jumanne,Jumatano,Alhamisi,Ijumaa,Jumamosi na Dominica?Nithibitishie ili niache ujinga?Halafu ukimaliza hilo uniambie Yesu alitumia kalenda ipi kwa nyakati hizo.Samualeko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…