MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 924
- 1,096
Tunaweza kuondoka kwenye mfumo wa lawama kwa kuitazama hii fursa.
Hii ni ripoti ya uchambuzi wa kiujumla wa kiuchumi uliofanywa na Benki ya Stanbic kuhusiana na mradi wa gesi wa Lindi LNG.
Kwanza mradi huu umeonekana kuwa ni fursa nzuri ya kiuchumi na ya kipekee kabisa kuwahi kutokea.
Makadirio ni kuongeza pato la taifa.Itachangia ajira zaidi ya 277,000. Inategemewa kuwa soko la gesi litakuwa China, India, Singapore na Indonesia. mradi huu utaiweka Tanzania kwenye ramani ya wauzaji wa Gesi Duniani na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa tahadhari za masoko pia mikopo.
Kinachofuata kwasasa ni utekelezaji wa uwekaji mazingira wezeshi baada ya makubaliano na serikali.
Kwa Tanzania mradi utakuwa una manufaa kwa Ruvuma Corridor – Mikoa ya Lindi na Mtwara na inategemewa viwanda vya mbolea, viwanda vidogo vidogo, kilimo, na utalii vitaibuka na kufanya kuwepo kwa mapinduzi ya viwanda.
Miradi inayopangwa inategemewa kufikia uwekezaji wa hadi dola Billion 81. Kumbuka GDP yetu ni Dola bilioni 65.
Lindi LNG itakuwa na mkusanyiko wa makampuni na yanayounda huo mradi ikiwepo serikali ama TPDC (NewCo). TPDC wanatakiwa kuwa na hisa 12%.
Gharama ya mradi huu inakadiriwa kuwa US$25 billion ambapo 12% itamiliikiwa na serikali kupitia TPDC sawa na US$3.9 billioni – kiasi ambacho ni kikubwa kwa serikali na ambacho kinatakiwa kuangaliwa kitapatikana vipi
Issue ya msingi pia inayoongelewa ni namna gesi itakavyotumika ndani na nje ya kusafirishwa na wateja wake.
Ripoti imeangalia uwezekano wa Usafirishaji wa gesi kufikia masoko ya nchi Jirani na upanuzi wa reli ya SGR inayoweza kurahisisha usafiri.
Pia kuna haja kubwa ya kujenga uwezo wa biashara ndogondogo ili kuchukua fursa hii tarajiwa.
Ripoti imeshauri mambo kadhaa ikiwepo uharaka na umakini wa kufanya maaamuzi, kuimarishwa kwa miundombinu barabara na bandari, umeme (wa kujenga kiwanda).
Nawasifu Stanbic wamekuja na study nzuri. soma, chambua na angalia fursa – kuna wadau walishaanza kuiangalia hii fursa kwa mbali endeleeni.. angalia cha kufanya. malazi yatahitajika, umeme, huduma za jamii, hospitali (wanahitajika madaktari wapya zaidi ya 230), magari ya aina zote, chakula, nk.
Ukiwa na kampuni ukaanza kuwekeza japo kwa hasara kwenye kilimo ama usafirishaji fursa itakukuta.
TPDC kukusanya US$3.9billion wanagusa pengine soko la hisa.. unaweza pia kujiandaa kuwekeza.
View attachment Stanbic_LNG_Eng_SinglePages.pdf