Ndugu zetu Kenya, achaneni na mass testing

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Muelewe ya kuwa hata Tanzania tukisema tupimane wengi sana tutakutwa infected na corona. Jambo moja zuri ni kuwa sisi Waafrika hasa sie tuliopo katika Africa Mashariki nguvu ya virus huyu nguvu yake si kama ya Europe na continents nyingine, athari yake ni ndogo kwetu utakuta twaweza kutwa wengi tupo infected lakini hiyo haitusumbui ni ugonjwa ambao twaweza ishi nao na tukapona hata bila kwenda treatment.

Hivyo, hiyo mambo ya Mass testing itazidi kuwaweka katika panic, Lock down nayo itazidi kuwaweka ktk panic na kuumiza maisha ya watu wengi masikini, hata tukiangalia rate ya vifo Bado ipo chini sana hapa East Africa sasa kuweka knockdown ni kuzidisha taabu na panic ambayo ndiyo kitu kibaya sana.

Fuateni njia tunazotumia sisi Tz, fuateni njia za JPM pamoja tutashinda, lakini tuendelee kuchukua tahadhari.
 
Eti Knockdown, hiyo ndio gani tena? Tuacheni tufanye mambo yetu kwa utaratibu wetu. Kama nyie hamna huruma na baadhi ya wananchi wenzenu ambao tayari wana matatizo mengine ya kiafya na pia wakongwe, babu na bibi zenu au hata baba, mama, wajomba, shangazi au vijitoto vichanga endeleeni kuwatoa kafara, mkifata kiki ovyo za kisiasa.

Vifo hata vya watu 10 tu kwa sababu ambazo zinaweza zikazuia au zikaepukika ni hasara kubwa na laana pia kwa taifa lolote lile. Watu wanajitolea kupimwa kwa kupenda kwao, ili waweze wakawalinda wapendwa wao. Hata kuvaa barakoa tu, kuzingatia 'social distancing' na kunawa mikono mara kwa mara kwetu sisi waafrika, sanasana vijana, tunafanya ili kuwalinda wenzetu, sio sisi wenyewe.

Kuweni wastaarabu, acheni ubinafsi wa kipumbavu. Walisema wazee wa ndemi na mathathi kwamba majuto ni mjukuu, usingonje hadi yatakapokuandama ndio uanze kutilia maanani mambo ambayo yapo wazi kisayansi.
 

Mass testing haina maana kabisa sasa niambie mpaka muda huu mmepata faida gani kufanya iyo mass testing kama Matajiri wakubwa kama bill gates wamesha sema hio testing sio inshu tena bado mnahangaika ya nini kama mnajiona mko serious fanyeni kudevelop vaccine ili muwalinde hao wenye magonjwa nyemelezi mass testing haita punguza spread hata kidogo ndo mana CS Kagwe kila siku anakuja na namba kubwa zaidi, Convid is there to stay hakuna namna maisha lazima yaendeleee

Mmeamua kutumia kichaka cha corona mpate mikopo yenye nafuu sana mnasahau hata hio mass testing ni wastage of Resources
 
Nyinyi ndio wale ambao huwa mnaketi barabarani katikati kisa eti hamuwezi mkatembea huku mkitafuna karanga. Shughuli ya kutafuta tiba au vaccine inaendelea na tahadhari pia ya kuzuia maambukizi zaidi ikiendelea kuzingatiwa. Shirika la utafiti nchini Kenya, KEMRI, ni moja kati ya mashirika mengine duniani ambayo yamejisali na WHO ili kufanya jitihada za pamoja za kutafuta dawa/tiba. Nakuhakishia kwamba watu wataendelea kupimwa kote duniani hata baada ya kufifia kwa makali ya janga hil. Eti tumskize tajiri Bill Gates, ambaye anawaza tu kupiga hela ndefu za vaccine.
 
Achana na hiyo typing error....
Lakini ufahamu kua hata president wa South Africa ameongea kuwa haoni kama lock down inasaidia kitu..corona ingekua serious kama ilivyopita huko Spain na marekani tungekufa vibaya kama locusts kote hapa afrika mashariki
Hakuna hapa nchi ya kuweza kupambana na hii corona
 
tupeni takwimu za korona, acheni justification za usanii wenu...mie ni mtz halisi !
 
tupeni takwimu za korona, acheni justification za usanii wenu...mie ni mtz halisi !
Takwimu hazitakusaidia kitu zaidi utaongezewa panic wakati wewe immunity na environmental conditions zinakulinda
Kuna faida gani kupima watu 1000 then unapata Kati yao 25 ni + na hao positive baada ya wiki mbili wote wanakua safe! Pengine bila hata tiba ya maana!
(kwa afrika) Mass testing & lockdown ni wastage of time and money
 
Mass testing ingekua na maana kama kungekua na possibility ya ku test the whole count per single day, watu wote wakafikiwa then wale wako positive wangekua isolated... Hapo sasa hata namba yenu ingekua sahihi 98%..lakini Leo Kenya mfano wanatoa takwimu it's fine.. But hiyo namba inakosa maana kwa kua namba hiyo ni kwa hao waliobahatika kupimwa tu.. What about others?... Hii ni kusema Bado wapo wakenya wengi tu infected lakini wapo poa na hawana symptoms lakini wanaishi and even it happens you don't test them watakua na wataendelea kua vizuri tu....
Try to think hard about it...
 
We waache wanufaishe kundi la wapingaji kwenye wizara yao ya afya.
 
Waambie wapime naagonjwa mengine Kama typhoid na malaria washangae watu walivyo wagonjwa na wanapiga kazi
 
Tatizo hizo Ela za mkopo zilikua Ni kwa ajili ya mass testing na lockdown na vikao vya kutangaza matokeo (daily briefings)..wakiacha unafikiri kipi kitawatokea
 
umejuaje kama nita panic?! mie nataka nipewe takwimu ili nijue ukubwa wa tatizo hapa nchini kwetu...hii ni haki yangu kama raia.
usiniambie habari za "pengine"...huko ni kubashiri wakati hii ni karne ya 21 tunataka uhalisia.
 
Kitu ambacho huelewi ni kwamba Kenya haijakuwepo kwenye total lockdown(kama Uganda na S.A), tangia janga la Corona liibuke. Isipokuwa kwenye mitaa miwili tu, ya Eastleigh na Old Town. Gavana wa Mombasa Sultani Joho aliitisha Lockdown ila serikali kuu haikumkubalia. Sijui hizo propaganda zenu mlizitoa wapi. Isipokuwa 'travel restrictions' kwenye gatuzi tano tu shughuli mchana zinaendelea kama kawa, curfew ya kuanzia saa moja usiku ndio ipo kote nchini. Kitu cha pili ni kwamba Kenya inafanya targeted mass testing, yaani watu hawapimwi kwa mkupuo kiholela tu. Bali vipimo 'random' vinafanywa sehemu ambazo ni 'hotspots' za Corona, kama Namanga border.
 
umejuaje kama nita panic?! mie nataka nipewe takwimu ili nijue ukubwa wa tatizo hapa nchini kwetu...hii ni haki yangu kama raia.
usiniambie habari za "pengine"...huko ni kubashiri wakati hii ni karne ya 21 tunataka uhalisia.
Takwimu unaipata lakini si sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…