Ndugu zetu msio taka katiba na demokrasia tuelezeni sababu!

Ndugu zetu msio taka katiba na demokrasia tuelezeni sababu!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kuna watu hapa hawataki kusikia katiba mpya na wanaunga mkono wizi wa kura , hawasemi lolote watu kutekwa lakini cha ajabu wanasema wenyewe ni wazalendo.

Sasa watueleze sababu zao za kufikiria wanalitendea haki taifa hili. Cha ajabu wengine ni usalama wa taifa na Polisi!

Tupeni sababu zetu tujadili

Je ni pesa, uchawa kwa ndugu, kuunga mkono bila kuuliza, uchawa ambao hata wewe hujui sababu au unafikiria ni kwa manufaa ya taifa!

Mkikwepa haya majadiliano msitulaumu tukisema nyie ni mafisadi maana ndiyo sababu nyingine
 
Wasamehe bure ata wewe ukipewa mzinga huwezi kuona ubovu wa katiba unachopasawa kuelewa mtu mweusi ana roho mbaya saana na mfano wa shetani.unashangaa wachawi wanasifia Marais wetu Mimi sijawahi kuona raisi wa kusifia Tanzania hakuna jipya wanalofanya ni yaleyale tu uchuuzi.
 
Katiba mpya haijaleta mabadiliko Kenya.
Sio takwa la wananchi wenye shida nyingi kuwa na huu ulaghai unaoitwa katiba mpya au demokrasia.
Matakwa ya kweli ya wananchi yanatakiwa yaakisi tulichokipigania wakati wa kudai uhuru.
...
Maadui ni watatu tupambane nao
 
Katiba mpya haijaleta mabadiliko Kenya
Toa ushahidi mfano mdogo tu .

Diaspora wameongeza uwekezaji sana nenda kaone uwekezaji wa diaspora baada ya katiba.

Mahakama yao iko huru baada ya katiba

Serikali ya majimbo imeongeza huduma kwa jamii

Wewe tupe data zako mambo gani yalikuwa bora kenya kabla ya katiba na sasa si bora
 
Katiba mpya haijaleta mabadiliko Kenya.
Sio takwa la wananchi wenye shida nyingi kuwa na huu ulaghai unaoitwa katiba mpya au demokrasia.
Matakwa ya kweli ya wananchi yanatakiwa yaakisi tulichokipigania wakati wa kudai uhuru.
...
Maadui ni watatu tupambane nao

Mbona hata CCM wanakubali katiba ni muhimu wakienda kwenye makongamano lakini hakuna utekelezaji. Umuhimu wa katiba uko wazi kwa miaka zaidi ya 10 sasa
 
Toa ushahidi mfano mdogo tu .

Diaspora wameongeza uwekezaji sana nenda kaone uwekezaji wa diaspora baada ya katiba.

Mahakama yao iko huru baada ya katiba

Serikali ya majimbo imeongeza huduma kwa jamii

Wewe tupe data zako mambo gani yalikuwa bora kenya kabla ya katiba na sasa si bora
Huyo diaspora anayesubiri katiba mpya kuwekeza ni kilaza wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom