Ndugulile ataka Azimio la Bunge la kubinafsisha huduma ya vivuko Kigamboni

Ndugulile ataka Azimio la Bunge la kubinafsisha huduma ya vivuko Kigamboni

TikTok2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2022
Posts
1,816
Reaction score
3,150
Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile (Mb) ameliomba Bunge kupitisha azimio la kubinafsisha huduma za vivuko nchini.

Dkt Ndugulile aliyasema haya leo tarehe 31.01.2022 wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyowasilishwa mapema leo Bungeni, Dodoma.

Dkt. Ndugulile amedai kuwa Taasisi ya Temesa imeshindwa kusimamia na kuendesha huduma za vivuko Kigamboni, hali inayopelekea kuwepo kwa malalamiko ya mara kwa mara toka kwa wakazi wa Kigamboni wanaotumia huduma hii.

Dkt. Ndugulile ameitaka Serikali kuchukua hatua stahiki na kutosubiri maafa kabla ya kuchukua hatua.

Aidha, Dkt Ndugulile ameliomba Serikali kufanya mapitio ya zabuni ya ukarabati wa MV Magogoni ambayo inatarajiwa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya ukarabati. Dkt Ndugulile amesema kuna taasisi nchini zenye uwezo wa kukarabati na kujenga meli ndogo ndogo. Hivyo, kufanya ukarabati wa MV Magogoni nje ya nchi, utapelekea kufanya malipo kwa fedha za kigeni na kuathiri ajira ambazo zingetumika kwenye ukarabati huo.
 
Aidha, Dkt Ndugulile ameliomba Serikali kufanya mapitio ya zabuni ya ukarabati wa MV Magogoni ambayo inatarajiwa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya ukarabati. Dkt Ndugulile amesema kuna taasisi nchini zenye uwezo wa kukarabati na kujenga meli ndogo ndogo. Hivyo, kufanya ukarabati wa MV Magogoni nje ya nchi, utapelekea kufanya malipo kwa fedha za kigeni na kuathiri ajira ambazo zingetumika kwenye ukarabati huo.[emoji817][emoji818][emoji1752]
 
Mbunge wa Historia Huyu alimshinda Mwana Mfalme fulani enzi hizo! [emoji38]

Ilistua wengi na kuwa gumzo la Jiji.
 
Serikali iachana na hii biashara, ikusanye kodi - pale ni wizi mtupu, huduma hovyo, msongamano balaa.
 
Dkt Ndugulile amedai kuwa Taasisi ya Temesa imeshindwa kusimamia na kuendesha huduma za vivuko Kigamboni, hali inayopelekea kuwepo kwa malalamiko ya mara kwa mara toka kwa wakazi wa Kigamboni wanaotumia huduma hii.
Vivuko hivi ni mradi wa watu miaka nenda rudi, Mbunge umegusa maslahi ya wenyewe jiandae kwa mashambulizi.
 
Wabinafsishe kampuni ya Bibi yake inshinde zabuni
 
Kwa uendeshaji wa baadhi ya miradi nyeti kwa taifa, ni vyema serikali ingalifanya kupitia ushirikiano wa sekta za umma na binafsi (Public–Private Partnership) ama maarufu kama PPP, kuliko kuing'ang'ania kuiendesha kwa hasara ama kasoro nyingi sana.
 
Back
Top Bottom