BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,554
- 9,247
Hivi viumbe vya ajabu kweli kweli kamanda....duh!! walikosea sana kumchagua huyu ndugule, bora ya makonda.Badala ya kufikiria na wao waalike wataalamu wa kutengeneza mfumo wa simu za bei chee wao wanawaza wapi pa kupata hela...
Hivi viumbe vya ajabu kweli kweli kamanda....duh!! walikosea sana kumchagua huyu ndugule, bora ya makonda.
Sasa huyu naye, kila sehemu ni kubana tuWaziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Faustine Ndugulile amesema ukiangalia simu zinazopigwa kwenda nje au kuingia kutoka nje zimepungua...
Huyu ni hamnazo kabisa, hivi kweli msomi kiwango cha PhD hajui kwamba hiyo ni advancement katika technology!!!? Amekosa washauri wa kumwambia nini azungumze mbele ya hadhira?Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Faustine Ndugulile amesema ukiangalia simu zinazopigwa kwenda nje au kuingia kutoka nje zimepungua.
Amesema watu huzungumza na watu wa nje kupitia mitandao kama whatsapp, skype nk hivyo ni lazima serikali ichukue hatua kurekebisha hilo
Bora ata wewe umepata muda wa kuandika kwa busara kama ivo.. mi kila nkitaka comment yanakuja matusi tuu kichwan mwangu. Nimeona nikae tuu kimya, jamaa wanatuchukuria sisi mazuzu ile mbaya. So sad kwakwelkwa serikali ya ambayo imeshindwa kutengeneza au kuunda vitega uchumi vyake au kiwanda cha kufuma toilet paper na kutatua changamoto za maji na umeme kwa miaka 60....
Huyu ndiye alisifiwa na Polepole kuwa Kigamboni wamweweka jembe, jembele lenyewe butu namna hii!!!?Hii inakuja kuwa wizara mbovu kuliko wizara zote na Ndugulile anakuja kupotea kwenye ramani ya watu waliodhaniwa wana akili ndani ya ccm.
Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Leo ndiyo namwelewa aliyesema aliyesema jembe ni kwaajili ya kuchimba makaburi na nyundo kutengeneza majenezaNadhani mpaka hapo tumeshaelewana,
Lengo la Serikali ya wanyonge ni kuhakikisha inaongeza wanyonge zaidi, haitaki watu wapate urahisi sehemu yoyote,
Hakika siku ikisikia wanyonge wengi wameanza kula Milo mitatu kwa siku lazima ije na lake jambo hata kama ni kuleta nzige ili tu kuhakikisha wanyonge wa kugawiwa T-shirt na kuhudhuria mikutano yao wapo wa kutosha.
Nilipoona wanamsifia wakati wa uteuzi, nikajua atahamasisha zaidi matumizi ya ICT kwenye uendeshaji wa serikali na kukuza biashara to cut down costs, leo anakuja kulaumu teknolojia!!!Binafsi namuona huyu Waziri kama mshamba, kiherehere na Mwenye kujipendekeza tu. Hana msaada wowote wa kitaalam ktk Wizara.
Yy ni kudhibiti tuu. Haongelei Kasi ya Internet, connection ya Mkonga wa Taifa wa mawasiliano ktk familia (kama Kenya), nk
Nimemsikiliza mwanzo hadi mwisho, hivi watu wataachaje kukejeli kama mawazo yake yenyewe ndiyo hayo!!!!?Waziri Ndugulile amesema pia wanaangalia mfumo wa kuwawezesha kujua yanayozungumzwa katika mtandao ili kubaini matusi kejeli na utapeli unaoendelea kwa njia ya simu na meseji.
Amejipambanua ati vijana wetu wanajaribu kuweka mfumo wa kufilter blablabla... huyu hajajua nguvu ya technology bado, hajajiuliza kwanini wakati wa uchaguzi still watu walitumia vpn baada ya serikali kuziba njia!!!?3. Serikali isijaribu kushindana na teknolojia. Hakuna aliyewahi kushindana na teknolojia akashinda. Serikali ikitaka watu walipie kodi simu za Whatsapp, watu watatumia application zingine kupigia simu ndugu zao, kama vile Viber, Talkhome, Yola, Dingtone, TalkU etc. Na bado kila siku zinabuniwa nyingine mpya. Serikali haiwezi kutoza kodi zote.
Na ni mengi mno, kuanzia elimu, afya, miundombinu ambayo bado tupo nyuma mno, ustawi wa jamii, ufanisi, kazi kwa vijana na bei za vifurushi...Kuna mambo ya kitaifa ya msingi ya kujadili kama Kutafuta soko la mahindi wanajadili WhatsApp!!
Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
Sijui hata alimshindahe bashite kwenye Kura za maoni maana ni zaidi ya takataka...Nimemsikiliza mwanzo hadi mwisho, hivi watu wataachaje kukejeli kama mawazo yake yenyewe ndiyo hayo!!!!?
Mbunge Msukuma anaweza kuwa sahihi, aliosema kuna baadhi ya wasomi wanazidiwa akili na darasa la saba
Mimi ni CCM lakini kwa hili siwezi kukuunga mkono Mh. Waziri.Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Faustine Ndugulile amesema ukiangalia simu zinazopigwa kwenda nje au kuingia kutoka nje zimepungua...