Ndungai na Dkt. Tulia hawaelewani? Kila moja anafanya yake

Ndungai na Dkt. Tulia hawaelewani? Kila moja anafanya yake

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Kama itakumbukwa kupitia walioitwa wabunge 19 wa CHADEMA baada ya kufukuzwa uanachama, kumetokea sintofahamu inayowachanganya watanzania kutokana kauli za viongozi hawa wawili Spika wa bunge na Naibu wake.

Alisikika Naibu Spika akisema kua wabunge wale ni halali na kuwataka wabunge kuacha kuwaita kua hawana vyama, Naibu spika aliongeza ofisi ya spika hakupokea barua yeyote toka Chadema.

Ameibuka tena Spika bunge Job Ndugai na kusema kua walipokea kipeperushi huku akiongea kwa kujiamini kua yeye mzoefu amekaa bungeni muda mrefu hivyo kanuni anazijua sheria.

Swali la kujiuliza, hivi hawa viongozi kazi hawafanyi pamoja hali inayopelekea kila mtu mtu kutamka kila mtu chake?
 
Wewe ndiye hujawaelewa, sawa? Tukijuacho ni kwamba Spika ni msaliti wa nchi yetu; Tulia angali katika mstari.
 
Ufalme uliofitinika huo. Mnara wa babeli utaporomoka soon
 
Wagogo walianza kuharibiwa uwezo wa kufikiri na mzee Samweli.
 
Back
Top Bottom