NEC:VYAMA VYA SIASA LETENI WATAALAM WENU WA TEKNOLOJIA YA KOMPYUTA WAJIRIDHISHE NA MFUMO UTAKAOTUMIKA KUJUMLISHA MATOKEO
Na Joseph Ishengoma
Wa Tume ya taifa ya uchaguzi
Oktoba 31,2001, Watanzania
*wenye sifa za kupiga Kura watashiriki katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani
* watakao waongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Siku hiyo ni siku maalum na yapekee ambayo Mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18, nakujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na mwenye shahada ya kupiga kura atatumia haki yake Kikatiba kuwachagua viongozi atakaoshirikiana nao kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Kura anayotarajia kupiga Mtanzania mwenye sifa zilizotaja hapo juu, ndiyo nguvu pekee aliyonayo mwananchi ya kuamua hatma ya Taifa lake kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo. Mtanzania mwenye sifa, aliyetumia muda wake kujiandikisha katika Daftari le Kudumu la Mpiga Kura na anayependa maendeleo ya nchi yake,hana budi kushiriki katika tukio hili muhimu.
Jumla ya wapiga kura 20,136,588 ambapo wapiga kura 19,728,919 waliandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na 407,669 waliandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) wanatarajia kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uchaguzi ni tukio muhimu sana katika jamii yoyote ile inayozingatia utawala bora. Uchaguzi utakaofanyika oktoba 31,2001, unatarajia kuhitimisha kipindi cha kampeini kilichoanza tangu tarehe 20 Agosti,2010.
Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ilikutana na Viongozi wa Vyama Vya Siasa Jijini Dar Es Salaam na kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu. Pia katika mkutano huo Tume ilitaka kupata maoni mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Vyama hivyo yenye lengo la kuboresha uchaguzu huo ili uwe huru na wa haki na kukidhi matarajio ya Watanzania.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume yataifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji mstaafu Lewis makame aliwaambia viongozi hao kuwa sambamba na kunadi sera za vyama vyao, viongozi hao wanawajibika kwa wananchi wote wanaojitokeza kuhudhuria mikutano ya kampeini za uchaguzi katika k uhakikisha kunakuwepo na amani na utulivu wakati wote kama inavyoelekezwa katika maadili waliyotia saini.
Tume inaamini kwamba vyama vitaendelea kuheshimi na kufuata maadili hayo ili kipindi kilichobaki, kila chama kipate fursa nzuri ya kunadi sera zake katika mazingira ya utulivu na amani, alisema.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, hali hiyo itasaidia kuwavuta wananchi wengi kuhudhuria mikutano ya vyama bila kuogopa na kusikiliza kwa makini sera za vyama husika.
Hata hivyo Jaji Makame alitumia fursa hiyo kuwasii viongozi wa vyamavya siasa kuhakikisha wanawadhibiti washabiki na wafuasi wao ili wasifanye fujo katika mikutano ya kampeini. Taadhari hiyo inatokana na taarifa kuwa kuna baadhi ya wafuasi wa vyama, wamekuwa chanzo cha fujo na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Alisema, Viongozi wote wa vyama vya siasa watumie muda uliobaki kuwataka wafuasi wao kuwa watulivu na kujiandaa kwa ajili ya siku ya kupiga kura.
Akiwasilisha mada ya Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Katibu wa Tume Bwana Rajabu Kiravu, alieleza hatua mbalimbali za maandalizi zilizokwisha fanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hatua hizo ni pamoja na shughuli za kuandaa na kusafirisha vifaa, uchapishaji wa karatasi za kura uliofanywa na Kampuni ya Kalamazoo Secure Solutions ya Uingereza na maandalizi ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mengine ni uteuzi wa wagombea, kampeini za uchaguzi, ushirikishwaji wa wadau wa uchaguzi, maandalizi ya siku ya kupiga kura, watendaji wa vituo vya kupiga kura, ulinzi wa vituo vya kupiga kura, mawakala wa upigaji kura, mabadiliko ya muundo wa karatasi za kura, kujumlisha kura na kutangaza matokeo pamoja na mchango wa washiriki wa maendeleo na asasi zisizo za kiserikali.
Pia Bwana Kiravu alitumia fursa hiyo kujibu hoja mbalimbali zilizoulizwa na viongozi hao wa vyama vya siasa ikiwemo ile ya mkakati wa kutumia teknolojia ya kompyuta kuiba kura.
Alisema mfumo (system) utakaotumika kupokea matokeo ya awali kutoka majimboni unaojulikana kwa kitaalam kama
Result Management System (RMS) umebuniwa na wataalam wa Tume na ndio wanaouratibu. Kwa mujibu wa Bwana Kiravu, lengo la kuwa na mfumo huo ni kuharakisha zoezi la kujumlisha matokeo kutoka maeneo mbalimbali ilii wananchi wapate matokeo haraka, sio kuhujumu matokeo.
Kama vyama vina mashaka na mfumo huu, basi vilete wataalam wake wa kompyuta wakae na wataalam wa Tume na kujiridhisha jinsi unavyofanya kazi ili wasiwe na mashaka nao, alisema. Alifafanua kuwa katika dunia ya leo inayoongozwa na teknolojia, Tanzania haiwezi kuepuka matumizi ya teknolojia, ila kinachotakiwa ni vyama vyenyewe kujipanga na kuiarifu tume lini watakuja kujiridhisha na mfumo hu.
Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu utendaji kazi wa mfumo huo, Mkuu wa Idara ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dr. Sisti Cariah alisema, Tume itatoa kompyuta mbili kwa kila Halmashauri zitakazotumika kujumlisha na kuleta matokeo makao makuu ya Tume. Kompyuta hizo zitakuwa na namba maalum, hivyo haitakuwa raisi kompyuta nyingine tofauti na hizo kutuma matokeo ya uchaguzi makao makuu ya tume ya Uchaguzi.
Aidha kila wilaya itateua na kutuma wataalam wawili wa kompyuta makao makuu ya tume Dar Es Salaam kuhudhuria mafunzo ya kutumia mfumo huo wa kupokea matokeo.
Pamoja na kutumia mfumo huo, vyamavyote vya siasa vitapewa nakala ya matokeo katika vituo. Hivyo vyama navyo vinaweza kujumlisha na kupata matokeo sahihi alisema.
Kuhusu wanavyuo kuruhusiwa kupiga kura, Bwana Kiravu alisema kuwa Tume haina data base ya wanavyuo, ina data base ya wapiga kura. Daftari la Wapiga Kura halikuboreshwa wakati mmoja. Kuna mambo ambayo huwezi kuyafanya kiujumla na sasa hivi hatuwezi kulifumua kufanya mabadiliko yoyote vinginevyo uchaguzi hautafanyika. Tukubali kuwa watakaoshindwa kupiga kura sio wanavyuo peke yao.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa muundo wa karatasi za kura umebadilika.
Alisema kuwa muundo wa sasa, Mpiga kura baada ya kumaliza taratibu zote za kujitamblisha na kukabidhiwa karatasi za Kura, atatakiwa kuweka alama ya Vema inayoashiria amemchagua nani kwenye chumba kilicho wazi, kulia kwa picha ya Mgombea.
Hata akiweka alama hiyo katika picha, kura hiyo itatambuliwa kwasababu ameonyesha dhamira yake, alisema.
MWISHO.