Uchaguzi 2020 NEC: Lugha rasmi kwenye kampeni ni Kiswahili

Uchaguzi 2020 NEC: Lugha rasmi kwenye kampeni ni Kiswahili

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
6,710
Reaction score
9,063
Nimemsikiliza Katibu ya Tume ya Uchaguzi NEC Mr. Kawishe akihojiwa na Channel 10.

Huyu jamaa anazijua Sheria za NEC na moja ya sheria hizo ni kutumia lugha ya Kiswahili kama official language kwene Kampeni na mtu akitumia lugha zingine kama KABILA FULANI anakuwa amekiuka Maadili na anatakiwa awajibishwe.

Wakati mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Kanda ya Ziwa alitumia lugha ya Kisukuma, Kihaya, Kikurya n.k. kwenye majimbo yenye makabila husika!!

Swali ni Je, Tume ya Kawishe haikumsikia mgombea akibonga kilugha na ilimchukulia hatua gani?

 
Hivi mkuuu..! Unaweza kumchukulia hatua gani Rais wa nchi ambaye pia ndiye bosi wako?? Mbona mnapenda kuzua hoja zenye majibu ya kutumia "logic" tu?

nimepaniki kwakweli[emoji2955]
 
Hivi mkuuuu..! Unaweza kumchukulia hatua gani Rais wa nchi ambaye pia ndiye bosi wako?? Mbona mnapenda kuzua hoja zenye majibu ya kutumia "logic" tu?

nimepaniki kwakweli[emoji2955]
Acha uzezeta wewe!
Rais anatakiwa achukuliwe hatua kwa mjibu wa KATIBA na SHERIA za nji na siyo mtu fulani!
 
Ni kweli kabisa , lakini eeeh , unajua sisi Tume hatufanyi kazi na mitandao 😆😆😆
 
Wakati yule mgombea wa CCM akiwa kanda ya ziwa,sheria ilikuwa haijatungwa
NEC watakwambia wao huact based on malalamiko rasmi yanayopelekwa kwao kwa maandishi kutoka kwa wagombea wengine.

As long as hakuna aliyesubmit malalamiko, wao hawawezi kufanyia kazi kitu ambacho hakipo
 
NEC watakwambia wao huact based on malalamiko rasmi yanayopelekwa kwao kwa maandishi kutoka kwa wagombea wengine.

As long as hakuna aliyesubmit malalamiko, wao hawawezi kufanyia kazi kitu ambacho hakipo
Hayo ndo huwa tunasema yanawezekana ONLY IN TANZANIA!

Haiwezekani wewe utunge Sheria halafu ushindwe kuzisimamia.

Angelikuwa ameyafanya mgombea wa Chama cha✌️ saa hii angelikuwa amefungiwa mwezi mzima ati 🤣🤣
 
NEC imethirisha kuwa na mapungufu mengi sana uchaguzi huu nadhani hili linapelekea kurejesha hoja ya msingi ya kuwa na KATIBA mpya...najua hili la Katiba halipendwi kwa utawala wa awamu ya 5
 
Hivi mkuuuu..! Unaweza kumchukulia hatua gani Rais wa nchi ambaye pia ndiye bosi wako?? Mbona mnapenda kuzua hoja zenye majibu ya kutumia "logic" tu?

nimepaniki kwakweli[emoji2955]
Kwa watu wanajielewa huwa wanajiuzulu kwa kushindwa kutimiza wajibu....kwa lugha rahisi ni kwa kutowajibika.
 
Angekuwa wa upande mwingine angefungiwa wiki 7 asifanye kampeni, kwa kulonga ki-push...
 
Tungekuwa tunafuata haki na sheria basi kuna mgombea alitakiwa angalau afungiwe siku kadhaa kufanya kampeni kama sio kuenguliwa kabisa, tatizo ana mizizi iliyojichimbia kwa kwenda chini kuliko wagombea wengine.
 
Back
Top Bottom