Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Viongozi wengine wa Serikali hawapaswi kuingia vituo vya kupigia, kuhesabu au kujumulishia kura. Viongozi hao wanaruhusiwa kuingia vituoni kwa madhumuni ya kupiga kura tu.