NEC: Mawaziri, Wakuu wa mikoa na wilaya hawaruhusiwi kuingia kwenye vyumba vya kujumlishia kura!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Tume ya uchaguzi imesema mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na watumishi wengine wa umma hawaruhusiwi kuingia kwenye vyumba vya kupiga, kuhesabu na kujumlisha kura isipokuwa kwa ajili ya wao kupiga kura tu.

Chanzo: Mwanahalisi Digital

Maendeleo hayana vyama!

===========

WAKUU wa Mikoa (RC) na Wilaya (DC) nchini Tanzania, ni miongoni mwa watendaji wa Serikali ambao hawatakiwi kuingia katika vituo vya kupiga, kuhesabu au kujumlishia kura.

Marufuku hiyo ipo katika Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 kilichotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania.

Sehemu ya tatu kifungu cha 3.3 ya kitabu cha maadili, imebainisha mambo manne yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa Serikali wakati wa uchaguzi utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Mosi; mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuchanganya ziara za kikazi na shughuli za kiuchaguzi na kutumia vyombo au watendaji wa Serikali katika shughuli za uchaguzi kwa manufaa yao.

Pili; mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa Serikali kuingia katika vituo vya kupigia, kuhesabu au kujumulishia kura.

Isipokuwa kwamba mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa Serikali wanaruhusiwa kuingia katika kituo cha kupigia kura kwa madhumuni ya kupiga kura tu.

Kuhusu hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa NEC, Giveness Aswile amesema, maadili hayo yanapaswa kuzingatiwa na kila mmoja ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika na kumalizika salama.

Amesema, kama kuna mtu anakiuka maadili hayo mathalani wakuu hao wa mikoa na wilaya wataonekana katika chumba cha kuhesabu, kujumulisha na kutangaza matokeo wanaweza kukataa kwa kujaza fomu maalum ambazo zinakuwepo kulalamikia suala hilo.

Tatu; waziri au afisa mwandamizi yeyote wa Serikali kumwita msimamizi wa uchaguzi kwa lengo la kujadili masuala ya uchaguzi kuanzia kipindi cha kampeni mpaka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Nne; kuanzia kipindi cha kampeni za uchaguzi mpaka kutangazwa kwa matokeo, mawaziri hawaruhusiwi

I; kutangaza katika vyombo vya habari au kwa namna yoyote misaada au ahadi ya aina yoyote

II; kutoa ahadi za shughuli za maendeleo ya jamii kwa mfano, kujenga barabara, kusambaza maji na mambo mengine kama hayo kwa lengo la kuungwa mkono kisiasa

III; kutumia madaraka au rasilimali za Serikali kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kwa manufaa ya chama chochote au mgombea yeyote.
 
Je wagombea wanaruhusiwa kuingia kuangalia upigaji na uhesabuji wa kura? Au ni mawakala wao tu?
 
Watakuja kulalamika tena kwa hili[emoji16][emoji16] wana nongwa kweli kweli[emoji28][emoji28]
 
Hilo sawa na ni hatua moja muhimu. Hatua ya pili muhimu za ni uhesabuji huru na wa wazi wa kura zilizopigwa kwenye kila kituo kimoja, kata, jimbo na taifa kutegemeana na nafasi inayogombewa.
 
Tume ya uchaguzi imesema mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na watumishi wengine wa umma hawaruhusiwi kuingia kwenye vyumba vya kupiga, kuhesabu na kujumlisha kura isipokuwa kwa ajili ya wao kupiga kura tu.

Chanzo: Mwanahalisi Digital

Maendeleo hayana vyama!
Je, hii inasaidia kwa kiwango kipi kuufanya uchaguzi kuwa wa huru na haki? Ni kiini macho tu.
 
Kumbe ndio maana mkubwa aliitisha kikao na wale wakurugenzi husika. Ameshawaagiza cha kufanya
 
Wanasema hivyo Tuu lakini ukweli hata wakija kuingia hawatafanya chochote ni kutuweka maboya tuu, kutudanganya tuwaone wapo siriaz kumbe La....!!.
 
Basi Na iwe kwa mgombea yeyote (hata rais) asitoe ahadi kwa kipindi chore cha kampeini- to be fair
 
Watakuja kulalamika tena kwa hili[emoji16][emoji16] wana nongwa kweli kweli[emoji28][emoji28]
Acha ufala basi wewe mama! Aaarrgghh kwa Kassim Majaliwa yeye huko anakozunguka huwa anafanya kitu gani? Kwani wewe hujasikia akitoa ahadi kibao!? Acheni undezi maana kila kitu kwenu mnachukulia mashkara.
 
Tume ya uchaguzi imesema mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na watumishi wengine wa umma hawaruhusiwi kuingia kwenye vyumba vya kupiga, kuhesabu na kujumlisha kura isipokuwa kwa ajili ya wao kupiga kura tu.

Chanzo: Mwanahalisi Digital

Maendeleo hayana vyama!

===========

WAKUU wa Mikoa (RC) na Wilaya (DC) nchini Tanzania, ni miongoni mwa watendaji wa Serikali ambao hawatakiwi kuingia katika vituo vya kupiga, kuhesabu au kujumlishia kura.

Marufuku hiyo ipo katika Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 kilichotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania.

Sehemu ya tatu kifungu cha 3.3 ya kitabu cha maadili, imebainisha mambo manne yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa Serikali wakati wa uchaguzi utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Mosi; mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuchanganya ziara za kikazi na shughuli za kiuchaguzi na kutumia vyombo au watendaji wa Serikali katika shughuli za uchaguzi kwa manufaa yao.

Pili; mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa Serikali kuingia katika vituo vya kupigia, kuhesabu au kujumulishia kura.

Isipokuwa kwamba mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa Serikali wanaruhusiwa kuingia katika kituo cha kupigia kura kwa madhumuni ya kupiga kura tu.

Kuhusu hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa NEC, Giveness Aswile amesema, maadili hayo yanapaswa kuzingatiwa na kila mmoja ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika na kumalizika salama.

Amesema, kama kuna mtu anakiuka maadili hayo mathalani wakuu hao wa mikoa na wilaya wataonekana katika chumba cha kuhesabu, kujumulisha na kutangaza matokeo wanaweza kukataa kwa kujaza fomu maalum ambazo zinakuwepo kulalamikia suala hilo.

Tatu; waziri au afisa mwandamizi yeyote wa Serikali kumwita msimamizi wa uchaguzi kwa lengo la kujadili masuala ya uchaguzi kuanzia kipindi cha kampeni mpaka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Nne; kuanzia kipindi cha kampeni za uchaguzi mpaka kutangazwa kwa matokeo, mawaziri hawaruhusiwi

I; kutangaza katika vyombo vya habari au kwa namna yoyote misaada au ahadi ya aina yoyote

II; kutoa ahadi za shughuli za maendeleo ya jamii kwa mfano, kujenga barabara, kusambaza maji na mambo mengine kama hayo kwa lengo la kuungwa mkono kisiasa

III; kutumia madaraka au rasilimali za Serikali kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kwa manufaa ya chama chochote au mgombea yeyote.

Waache kutamka tu, wasimamie hayo matamko. Kwanza kwanini Majaliwa anafanya kampeni za urais? Mgombea anaweza kuwa kwenye kampeni za mgombea mwingine? Mbona hamjatoa tamko wala kumsimamisha? Mahera upo?
 
Back
Top Bottom