Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Kinyume na makubaliano kati ya vyama vya siasa na NEC katika dakika za lala salama kuelekea uchaguzi NEC wamegoma kuwalipa mawakala na kuwatupia zigo hilo vyama husika.
Leo kiongozi mmoja wa NCCR MAGEUZI alionekana Channel Ten jioni hii akilia na NEC kwa kukiuka makubaliano yake na vyama vya siasa.
Zimekuwepo shutuma nyingi dhidi ya NEC kuyachakachua matokeo na kuwanufaisha CCM na hili ni jipu jingine ambalo laweza kupasuka wakati wowote ule.
Mawakala wa vyama vya siasa ndiyo inasadikiwa ni karata turufu ya kumwokoa JK na CCM kutoka kwenye kibanio cha kudhalilishwa vibaya na Chadema kwenye chaguzi hii.
Hivyo kutowalipa mawakala yawezekana kabisa kuwa ni njama ya kuwaweka mawakala hao katika hali ya tafurani ambayo endapo vyama vyao vikishindwa kuwalipa CCM ikawalipa na hivyo kuzua utata wa wanawajibika kwa nani na hivyo kuufanya uchaguzi huu kutokuwa wa huru na wa haki.
Pamoja na Mwenyekiti wa NEC kuahidi chaguzi hii kuwa ya huru na haki yapo matendo mengi ya NEC yanayoashiria kuwa nia hii siyo ya dhati na kutoka moyoni.
Zimekuwepo kauli za kutofautiana kati ya NEC na wasimamizi wa chaguzi majimboni na hili NEC imeshindwa kuwakemea wasimamizi hao au hata kutoa mwongozo unaoeleweka hususani kwenye eneo la wapigakura kuwa mita 100 kutoka vituo vya kuhesabia kura kuhakikisha haki inatendeka........Msimamizi wa Tarime amedai wapigakura wajiendee majumbani na watajulishwa matokeo jambo ambalo Naibu Mwenyekiti wa NEC tayari alikwisha kutoa mwongozo tofauti kabla ya hapo alipouulizwa swali na mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini Bw. Rwakatare..........NEC walisema ni ruhksa kwa wapigakura kuwa mita 100 kutoka vituo vya kupiga kura............